Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Mhe. Kanali Patrick Kenan Sawala, ameelezea Maonesho ya Madini ya Lindi Mining Expo 2025 kama nguzo muhimu ya maendeleo ya kiuchumi kwa mikoa ya kusini.
Akizungumza leo tarehe 12 Juni 2025, wakati wa kufungua mafunzo ya wadau wa madini mkoani Lindi, Kanali Sawala amesema kuwa hatua hii imefungua milango ya uelewa, ushirikiano, na uwekezaji kwenye sekta ya madini.
“Mkoa wa Lindi ni miongoni mwa wazalishaji wakubwa wa madini nchini. Kupitia maonesho haya, wananchi na wawekezaji wamepata fursa ya kujionea utajiri mkubwa uliopo na kuchangia katika maendeleo ya uchumi wa kusini,” amesema.
Aidha, amewahimiza wachimbaji wadogo kutumia maarifa wanayopata ili kuongeza tija, huku akisisitiza kuwa mashirikiano kati ya Mikoa ya Lindi na Mtwara yameendelea kuzaa matunda chanya kwa sekta ya madini.
LINDI MINING EXPO 2025 si tukio tu, ni jukwaa la mabadiliko kwa uchumi wa wananchi na taifa kwa ujumla.
Kilwa Masoko
Anuani ya Posta: 160
Simu: 0672365354
Simu: 0672581557
Barua pepe: ded@kilwadc.go.tz /ictsupport@kilwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa