katika kuadhimisha miaka 63 ya Uhuru wa Tanzania Bara, Wilaya ya Kilwa imefanya Kongamano la Uhuru Wilayani humo kwa lengo la kuwakutanisha wadau mbalimbali kufanya majadiliano juu ya miaka 63 ya Uhuru, kujadili juhudi mbalimbali zinazofanywa na serikali katika kuboresha maisha ya watanzania na kupata historia ya uhuru wa Tanzania Bara.
Kongamano hilo limefanyika katika ukumbi wa Shule ya Sekondari Ilulu likiwa na bahati ya kupata watoa mada adhimu waliokuwepo kipindi cha uhuru wakiongozwa na Mhe. Balozi Ally Mchumo,
Kauli mbiu ya Kongamano hilo ni,
Miaka 63 ya Uhuru wa Tanzania Bara.
"Uongozi madhubuti na ushirikishwaji wa wananchi ni msingi wa maendeleo yetu".
Kilwa Masoko
Anuani ya Posta: 160
Simu: 0672365354
Simu: 0672581557
Barua pepe: ded@kilwadc.go.tz /ictsupport@kilwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa