Timu ya Menejimenti ya Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa (CMT), ikiongozwa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri, Ndg. Abushiri Mbwana, imefanya kikao muhimu cha tathmini na ufuatiliaji wa utekelezaji wa shughuli za maendeleo kwa kila Idara na Kitengo.
Kikao hicho kimefanyika tarehe 14 Aprili 2025 katika Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji na kililenga kujadili mafanikio, changamoto na mikakati ya kuboresha utekelezaji wa majukumu kwa kipindi cha Robo ya Tatu (Januari – Machi) ya Mwaka wa Fedha 2024/2025.
Kupitia kikao hiki, CMT imeweka msisitizo katika kuhakikisha matumizi bora ya rasilimali, uwajibikaji wa watendaji, na kuongeza kasi ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa manufaa ya wananchi wa Wilaya ya Kilwa.
Aidha Ndg. Abushiri amesisitiza suala la Ushrikiano baina ya watumishi ili kufikia dhamira walizojiwekea kama uwajibikaji,kutunza rasilimali ili kuleta maendeleo kwa jamii ya Kilwa na Taifa kwa Ujumla.
Kilwa Masoko
Anuani ya Posta: 160
Simu: 0672365354
Simu: 0672581557
Barua pepe: ded@kilwadc.go.tz /ictsupport@kilwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa