Klabu ya Mazoezi na Kukimbia ya Kilwa(Kilwa Fitness Jogging) kwa kushirikiana na Taasisi ya Umoja Pamoja Leo Tarehe 12/04/2025 wamefanya shughuli ya utunzaji wa mazingira kwa kupanda Miti ya Mikoko katika maeneo ya Baharini Kilwa Masoko lengo ikiwa ni kuongeza uelewa kuhusu umuhimu wa mimea kwa jamii ya Kilwa.
Zoezi hilo limeratibiwa kwa ushirikiano wa wadau mbalimbali wa Maendeleo wakiwemo Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), shirika la ActionAid pamoja na Kitengo cha Utamaduni, Sanaa na Michezo ikiwa ni sehemu ya juhudi za pamoja za kulinda Mazingira ya Pwani na kukabiliana na athari za mabadiliko ya Tabianchi.
Waratibu wa tukio hilo wamesisitiza kuwa ushirikiano wa kijamii katika kulinda Mazingira ni hatua muhimu kuelekea Maendeleo endelevu, pia Wananchi wamehamasishwa kuendelea kushiriki katika shughuli za Maendeleo ya kijamii kwa manufaa ya kizazi cha sasa na baadae.
Kilwa Masoko
Anuani ya Posta: 160
Simu: 0672365354
Simu: 0672581557
Barua pepe: ded@kilwadc.go.tz /ictsupport@kilwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa