Uongozi wa Kitongoji cha Miembe Miwili na Wataalamu kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa umefanya Mkutano wa Kijiji kujadili juu ya Maendeleo Ujenzi wa Uwanja wa Michezo unaojulikana kwa jina la Uwanja wa Mwenge (Taifa) kupitia Fedha za Mfuko wa Jimbo Milioni10 zilizoingizwa hivi karibuni.
Mkutano huo umefanyika Tarehe 21/03/2025 katika Uwanja wa Mwenge (Taifa) ambapo Viongozi na Wataalam hao wamekutana na Wananchi ili kujadili namna ya kuendesha Ujenzi wa Uwanja huo kwa kuunda kamati ya Wataalamu na Wajumbe wa mkutano huo watakao simamia ujenzi, hii ni mara baada ya kuingia kwa fedha za Mfuko wa Jimbo Shilingi Milioni 10 kwaajiri ya kuendeleza ujenzi wa Uwanja huo.
Akizungumza katika Mkutano huo Diwani Kata ya Masoko Mhe. Haji Chijinga Ameishukuru serikali ya Awamu ya Sita kuwaingizia fedha katika utekelezaji wa Miradi Mbalimbali ikiwemo wa Ujenzi wa Uwanja wa Mwenge (Taifa), huku akizitaka Kamati za Wataalamu na Wajumbe zilizoundwa katika Mkutano huo kushrikiana kuhakikisha mradi huo unakamilika na fedha hizo zinatumika vizuri.
Kwa Upande Wake Afisa Utamaduni Sanaa na Michezo Wilaya ya Kilwa Bi. Veneranda Maro ametoa rai kwa wananchi kushirikiana na Viongozi katika kuulinda uwanja wa Mwenge (Taifa) kwa maslai mapana ya vijana wanaotumia uwanja huo katika kuibua Vipaji vyao kimichezo ili waweze kufika malengo yao.
Kilwa Masoko
Anuani ya Posta: 160
Simu: 0672365354
Simu: 0672581557
Barua pepe: ded@kilwadc.go.tz /ictsupport@kilwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa