Kilwa,
Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa imeendelea kutekeleza agizo la Waziri wa nchi ofisi ya Rais (Tamisemi) Mhe. Seleman Jafo la kutumia Mfumo wa taifa wa kuhifadhi taarifa Hospitalini GoTHoMIS katika haspitali na vituo vya afya Nchini.
Akizungumza baada ya kukamilika kwa ufungaji wa Mfumo huo katika Kituo cha afya Masoko, Afisa Tehama kutoka ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi Ndg. Denis Venance ambaye ndiye msimamizi wa zoezi hilo amesema zoezi la ufungaji Mfumo limekamilika na umeanza kutumika rasmi katika kutoa huduma kwa Wanachi.
“Jumatatu tulianza kufanya installation katika sever kubwa, tuliweka dawa katika mfumo, tuliweka procedure, vipomo vyote na tuli set price.
Jumanne na jumatano tukafanya mafunzo kwa watumishi juu ya matumizi ya mfumo huu na jana Alhamisi tulimalliza mafunzo na kuanza rasmi matumizi ya mfumo” alisema Denis.
Denis amewatoa hofu Wananchi juu ya matumizi ya mfumo, amesema watumishi wamepatiwa mafunzo ya kutosha juu ya matumizi ya mfumo na kuahidi kuimarika kwa huduma.
“Kama nilivyo tangulia kusema kuwa kuanzia Jumanne hadi jana tulikuwa tunafanya mafunzo juu ya matumizi ya mfumo kwahiyo watumishi wameuelewa na kuanzia sasa wategemee mabadiliko” alisema Denis
Denis amebainisha mabadiliko yatakayopatikana kutokana na mfumo huo ni pamoja na kuongezeka kwa mapato baada ya kudhibiti mianya yote kupoteza mapato,upatikananji wa takwimu sahihi za wagonjwa , matumizi ya dawa na nyinginezo nyingi.
Aidha amewataka watumishi kufanya mazoezi ya mara kwa mara ya kuutumia mfumo ili kuwaongezea kasi na ufanisi katika kutekeleza majukumu yao.
Kwa upande wake Mganga Mfawidhi Kituo cha afya Masoko Dokta Daudi Selemani ameshukuru wadau wote ambao wamefanikisha kukamilika kwa zoezi hilo ikiwemo kampuni ya gesi ya Songas pamoja na Mradi wa uimarishaji mifumo ya sekta za umma( ps3) kwa ushirikiano wao hadi kukamilika kwa zoezi hilo.
Aidha amewataka Wananchi kuwa wavumilivu katika kipindi hiki cha mpito ambapo kituo kina badili mfumo wa utoaji huduma kutoka Analojia kwenda Digitali.
“Tunaomba Wananchi wawe wavumilivu katika kipindi hiki kwani spidi ya huduma itapungua kidogo kutokana na matumizi ya mfumo lakini tumejipanga kuhakikisha huduma zinaendelea kwa spidi ile ile na nina imani ndani ya wiki ijayo kila kitu kitakuwa sawa” alihitimisha Dokta Daudi.
Kilwa Masoko
Anuani ya Posta: 160
Simu: 0672365354
Simu: 0672581557
Barua pepe: ded@kilwadc.go.tz /ictsupport@kilwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa