Kilwa,
Halmashauri ya wilaya ya Kilwa imesaini Mkataba wa lishe.
Mkataba huwo umesainiwa leo Disemba 4 na Mkuu wa wilaya, Katibu tawala na Mkurugenzi kwa niaba ya Halmashauri mbele ya Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Kilwa Mheshimiwa Abuu Mussa Mjaka Mjini Kilwa Masoko.
Akizungumza katika utiaji saini wa mkataba huo Mkuu wa Wilaya ya Kilwa Mheshimiwa Christopher Ngubiagai amewataka Wananchi kutumia Chumvi yenye madini joto pamoja na Wajawazito kuhudhuria Kliniki kwa wakati na kuafuata taratibu zote za kiafya ikiwemo matumizi ya Madini Chuma yanayotolewa kwa wajawazito.
Aidha amaeikumbusha Halmashauri kuingiza katika bajeti kiasi cha pesa kwa ajili ya shughuli za lishe ambapo Kila mtoto anatakiwa kutengewa kiasi cha Shilingi elfu moja.
Kwa upande wake Afisa Lishe Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa Bi. Veronica Barua ameziomba idara mbalimbali pamoja na taasisi za kiserikali na zisizo za kiserikali ziendelee kutoa ushirikiano katika suala zima la Lishe ili kuondoa matatizo yatokanayo na ukosefu wa lishe ikiwemo utapia mlo katika jamii.
Kilwa Masoko
Anuani ya Posta: 160
Simu: 0672365354
Simu: 0672581557
Barua pepe: ded@kilwadc.go.tz /ictsupport@kilwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa