Kilwa,
Halmashauri ya wilaya ya kilwa imepongezwa kwa kua miongoni mwa halmashauri zinazo ongoza kwa utoaji taarifa kupitia tovuti.
Pongezi hizo zimetolewa na Mtafiti mwandamizi kutoka taasisi ya Urban Institute ya nchini Marekani Dokta Fenohasina Rakotondrazaka Maret, alipotembelea halmashauri hio kukagua maendeleo ya mradi pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili katika kutekeleza majukumu yao.
Dkt. Fenohasina amesema wao kama wasimamizi wa mradi wamefurahishwa na utendaji wa halmashauri ya wilaya ya kilwa katika swala zima la kuhabarisha wananchi kuhusiana na matukio na miradi mbalimbali inayotekelezwa na halmashauri kupitia tovuti kama ilivyo agizwa na Waziri wa nchi, Or- Tamisemi Mhe. Selemani Jafo kua tovuti ziwe majokofu ya habari na si magofu ya habari.
“Tumefurahishwa na muenendo wa halmashauri katika swala zima la matumizi ya tovuti katika kuwa habarisha wananchi juu ya mambo mbalimbali kuhusiana na halmashauri yenu
Sana sana tumefurahishwa na uwazi juu ya taarifa mbalimbali, mfano nimeona bajeti ya halmashauri kwa mwaka wa fedha 2017/18 ikiwa imewekwa katika tovuti ambapo kila mwananchi anaweza kuona lakini pia tumeona miradi mbalimbali inayotekelezwa na Halmashauri pamoja na thamani zake lakini tumefurahishwa zaidi na jinsi mnavyoitangaza tovuti yenu” alisema Bi. Fenohasina
Aidha ameitaka halmashauri iendelee na kasi hio ili izidi kua mfano bora kwa tovuti zinginae za Mamlaka ya serikali za mitaa.
Kaimu mkuu wa kitengo cha teknolojia ya habari na mawasiliano Bw. Yusuph Rajabu (Katikati) akifafanua jambo kwa wajumbe kutoka Mradi wa uimarishaji Mifumo ya sekta za Umma (PS3) walipotembelea Halmashauri ya wilaya ya Kilwa kukagua maendeleo ya mradi pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili.
Akiwashukuru kwa ujio wao Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Kilwa Bw. Sylivester Mashema amesema amefurahi na anashukuru kwa ujio wao na kusikia changamoto mbalimbali zinazowakabili na kuahidi kuendelea kushirikiana na kitengo cha Tehama na idara zingine katika kuhakikisha wananchi wanapata habari sahihi na kwa muda sahihi.
“Nashukuru kwa uji wenu na kusikiliza changamoto zinazotukabili licha ya mafanikio tunayo yapata, na sisi kama halmashauri tutaendelea kushirikiana na kitengo cha Tehama kuhakikisha tunawahabarisha wanachi kuhusiana na mambo mbalimbali” alisema Mashema
Kwa upande wake Kaimu mkuu wa kitengo cha Teknolojia ya habari na mawasiliano (TEHAMA) Bw. Yusuph Rajabu amesema wamejipanga kuhakikisha kua wananchi wana habarika kupitia tovuti ya halmashauri na vyanzo vingine vya habari vinavyo simamiwa na Halmashauri.
Pia amewataka wananchi kushirikiana na Halmashauri kwa kuwasilisha malalamiko yao kupitia tovuti ya Halmashauri ili yapatiwe ufumbuzi kwa maendeleo ya Wananchi.
“Tume anzisha mfumo wa kupokea malalamiko kupitia tovuti kwakua tumeona wananchi wengi walioko mbali na Ofisi za Halmashauri inakua ngumu kwao kuwasilisha malalamiko yao moja kwa moja au kupitia sanduku la maoni ambalo mara nyingi hupatikana maofisini tu
Mfano mtu alie kuepo Kipatimu huko anawezaje kufikisha malalamiko yake kwa urahisi ofisini kwa mkurugenzi? Itamlazimu atumie gharama kuja mpaka wilayani na kurudi kwa kuliona hilo tumeanzisha mfumo maalumu wa kupokea malalamiko yao ambapo ataenda kwenye simu yake au kompyuta iliyounganishwa na huduma ya intaneti na kuandika neno www.kilwadc.go.tz itafunguka katika muonekano huu
Baada ya hapo utabofya sehemu ya kwanza ilio andikwa Malalamiko na itafunguka kama inavyo onekana hapo chini
Mlalamikaji ataweka malalamiko yake kwa kujaza taarifa na mwisho atamaliza kwa kuituma kwa kubofya sehemu ilio andikwa Send na malalamiko yake yatapokelewa moja kwa moja na kufanyiwa kazi.
Ila niwakumbushe tu kua malalamiko yawe na ukweli yasiwe ya uzushi kwa nia ya kuchafua mtu au idara fulani kwa sababu binafsi, isije kutokea mtu amekosana na mtumishi katika mambo yao binafsi akayaleta kama malalmiko kwa ajili ya kumkomoa au kumchafua" alisisitiza Bw. Yusuph.
Halmashauri ya wilaya ya kilwa ni Halmashauri ya kwanza kwa kua na watembeleaji wengi katika tovuti katika mkoa wa lindi ikiwa na watembeleaji zaidi ya 2620 ikifuatiwa na halmashauri ya wilaya ya Ruangwa yenye watembeleaji 670.
Kilwa Masoko
Anuani ya Posta: 160
Simu: 0672365354
Simu: 0672581557
Barua pepe: ded@kilwadc.go.tz /ictsupport@kilwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa