Katika kuendeleza ziara ya mafunzo mkoani Tanga, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa, Ndg. Hemed S. Magaro, akiambatana na baadhi ya wataalamu, viongozi wa BMU pamoja na viongozi wa Mtandao wa BMU Kilwa, wameendelea na ziara ya mafunzo katika Halmashauri ya Wilaya ya Mkinga, Tanga tarehe 24 Juni, 2025.
Lengo kuu la ziara hii ni kujifunza mbinu bora za ukusanyaji wa mapato ya baharini kupitia BMU pamoja na kujengewa uwezo katika masuala ya uhifadhi wa mazingira ya bahari.
Katika mafunzo haya, BMU kutoka Mkinga wameelezea kwa kina teknolojia ya utengenezaji wa matumbawe bandia na faida zake, ikiwa ni njia endelevu ya kulinda mazalia ya samaki na kuboresha mfumo wa ikolojia ya bahari.
Akizungumza mwishoni mwa ziara hiyo, Ndg. Magaro ameishukuru Halmashauri ya Mkinga kwa elimu waliyopatiwa na kusisitiza kuwa teknolojia ya matumbawe bandia itakwenda kuenziwa na kutekelezwa Kilwa kama hatua ya kulinda bahari na kuongeza uzalishaji wa rasilimali za uvuvi
Kilwa Masoko
Anuani ya Posta: 160
Simu: 0672365354
Simu: 0672581557
Barua pepe: ded@kilwadc.go.tz /ictsupport@kilwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa