Kilwa,
Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa imeushukuru Mradi wa uimarishaji mifumo ya sekta za umma (Ps3) kwa misaada inayoendelea kuipatia.
Akitoa shukrani kwa niaba ya Halmashauri wakati wa makabidhiano ya vifaa vya kiufundi kwa ajili ya maafisa Tehama kutoka Mradi wa uimarishaji mifumo ya sekta za umma, Kaimu Mkurugenzi Bw. Sylivester Mashema emesema Halmashauri inashukuru kwa misaada inayoendelea kutolewa na Mradi.
“Halmashauri inaushukuru mradi kwa kuendelea kuwa nasi bega kwa bega katika kuhakikisha mifumo tunayotumia ina imarika na inaleta tija kwa umma, na tunaomba muendelee na moyo huo kwani Halmashauri bado inategemea mengi kutoka kwenu” alisema Mashema.
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa Ndg. Sylivester Mashema (Kulia) akipokea Begi la vifaa vya kiufundi kutoka kwa Meneja wa Mradi wa uimarishaji mifumo ya sekta za umma Mkoa wa Lindi Bw. Aloyce Mwasuka ofisini kwake Mjini Kilwa Masoko (Picha: Ally Ruambo)
Nae Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama) Ndg. Yusuph Rajabu amesema anashukuru mradi kwa msaada wa vifaa kwani vitaongeza chachu ya ufanyaji kazi na kuahidi kuvitumia kwa uangalizi wa hali ya juu ili viweze kudumu kwa muda mrefu.
“Kabla tulikua na changamoto kidogo ya upungufu wa baadhi ya vifaa katika utendaji kazi wetu wa kila siku, kwa vifaa hivi vitasaidia sana kupunguza changamoto na kuongeza ufanisi katika kazi zetu na tuta vitunza zaidi ya mboni za macho yetu ili viweze kudumu na kutumika kwa muda mrefu” alisema Yusuph.
Kwa upande wake Meneja wa Mradi wa uimarishaji mifumo ya sekta za umma Mkoa wa Lindi Bw. Aloyce Mwasuka amewata maafisa Tehama kuvitumia vifaa hivyo katika kuimarisha mifumo ili ilete matokea chanya kama mradi ulivyokusudia.
Kilwa Masoko
Anuani ya Posta: 160
Simu: 0672365354
Simu: 0672581557
Barua pepe: ded@kilwadc.go.tz /ictsupport@kilwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa