Katika kuadhimisha Miaka 61 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar tangu mwaka 1964, Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa imefanya zoezi la usafi wa mazingira na upandaji miti katika Kituo cha Afya Masoko katika kuuenzi Muungano huo.
Zoezi hilo limehusisha ushiriki wa viongozi kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa, watumishi wa umma pamoja na wananchi, ikiwa ni sehemu ya kuuenzi Muungano huo wa kihistoria na kuunga mkono juhudi za uhifadhi wa mazingira na afya ya jamii.
Akizungumza Watumishi na Wananchi hao Katibu Tawala wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa Ndg. Yusuf Mwinyi, amewataka wananchi kuendelea kushiriki katika shughuli za kijamii na maendeleo pia amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuleta maendeleo kwa wananchi kupitia fedha za miradi mbalimbali ya kijamii.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, Ndg. Hemedi Magaro, amewapongeza watumishi na wananchi walioungana kushiriki katika zoezi hilo kwa mshikamano huo na kuonyesha dhamira ya kweli ya kuunga mkono Muungano na kulinda mazingira.
Kilwa Masoko
Anuani ya Posta: 160
Simu: 0672365354
Simu: 0672581557
Barua pepe: ded@kilwadc.go.tz /ictsupport@kilwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa