Kilwa,
Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa imeendelea kuunga mkono kauli ya Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli ya kuifanya Tanzania kuwa Nchi ya viwanda.
Kauli hiyo imetekelezwa leo juni 5 baada ya Katibu tawala Mkoa wa Lindi Ndg. Ramadhani Kaswa kuweka jiwe la msingi katika kiwanda cha kuchakata magogo cha Sound and Fair katika kijijji cha Nanjirinji wilayani kilwa kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe. Godfrey Zambi.
Akizungumza wakati wa uwekaji wa jiwe hilo la msingi Ndg. Kwasa amesema amefurahi kuona kampuni ya Sound and Fair inaunga mkono serikali ya awamu ya tano chini ya Mhe. Magufuli ya kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda na kuahidi kuendelea kutoa ushirikiano kwa kampuni hiyo na nyingine ambazo zinahitaji kuwekeza katika Mkoa wa Lindi.
“Nimefurahishwa na jitihada zenu za kuhakikisha kua Tanzania inakua nchi ya viwanda kwa kuanzisha kiwanda hiki cha kuchakata magogo, sisi kama mkoa tunaahidi kuendelea kuwapa ushirikiano na wale wengine ambao wanataka kuja kuwekeza katika Mkoa wa lindi tunawakaribisha” alisema Kaswa.
Katibu tawala Mkoa wa Lindi Ndg. Ramadhan Kaswa (wa pili kutoka kushoto) akikata utepe kuashiria kuwekwa rasmi kwa jiwe la Msingi katika Kiwanda cha Sound and Fair katika kijiji cha Nanjirinji, kutoka kulia ni Katibu tawala Wilaya ya Kilwa Ndg.Haji Mbaruku akifuatiwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Uchumi, Ujenzi na Mazingira Mhe. Msati.
Pia ameipongeza Kampuni ya sound and fair kwa kutoa ajira kwa vijna wa kitanzania pamoja na kuchangia pato la kijiji na taifa kwa ujumla kupitia kodi mbalimbali inayoendelea kuzilipa.
“Nimeona katika hotuba yenu kuwa hadi sasa mmekwisha lipa zaidi ya million 150 kutokana na kodi mbalimbali na mmetoa ajira kwa wataalamu mbalimbali kutoka hapa hapa Tanzania na wananchi kutoka vijiji vinavyo izunguka Nanjirinji na mnategemea kutoa ajira 60 za kudumu na zaidi ya 100 za muda mfupi jambo ambalo ni zuri kwani itasaidia sana kuongeza kipato cha vijana watakao ajiriwa” aliongeza Kaswa
Mkurugenzi wa kiwanda cha Sound and Fair Ndg. James Laizer (wa kwanza kulia) akitoa maelekezo kwa Katibu tawala Mkoa wa Lindi Ndg. Ramadhani Kaswa (katikati) na Mkuu wa Wilaya ya Kilwa Mhe. Christopher Ngubiagai (wa kwanza kushoto) ya jinsi mtambo unavyo fanya kazi walipo tembelea kiwandani hapo kuweka jiwe la msingi.
Nae mkuu wa wilaya ya Kilwa mhe Christopher Ngubiagai ameishukuru kampuni ya Sound and fair kwa uamuzi wao wa kuwekeza wilayani kilwa na kuwataka wananchi waache kuharibu Mazingira kwa kukata Miti, kuharibu vyanzo vya Maji na maeneo mbalimbali yalitengwa kwa ajiri ya hifadhi na kuahidi kuwachukulia hatua kali dhidi yao.
“Hatuwezi kuwafumbia macho ambao wanaharibu mazingira yetu kwa shughuli zao mbalimbali, kama nilivyosema jana wakati tunapanda Miti pale katika kijiji cha Makangaga kuwa serikali itawachukulia hatua kali ambao watakaidi agizo la kutoka sehemu zile ambazo haziruhuiswi kufanya shughuli yeyote ya kibinadamu” alisema ngubiagai
Katibu tawala Mkoa wa Lindi Ndg. Ramadhan Kaswa akipanda Mti katika kiunga cha Kiwanda cha Sound and Fair baada ya kuweka Jiwe la msingi.
Kwa upande wake mkurugenzi wa kampuni ya sound and fair Ndg. James Laizer ameiomba serikali kupitia mkuu wa mkoa kuwasaidia katika kurekebisha barabara ya Kiranjeranje mpaka Nanjirinji ambayo ndio muhimili mkubwa katika usafirishaji wa bidhaa ambazo zinaingia na kutoka kiwandani baada ya kuchakatwa.
Aidha Ndg. Laizer ameiomba serikali kuimarisha ushirikiano na wadau mbalimbali katika kutokomeza tatizo la uvunaji haramu wa mazao ya masitu ambayo imekua tishio kubwa kwa ustawi wa makampuni yanayojishughulisha na biashara ya mazao ya misitu.
Uwekaiji wa jiwa la msingi Katika kiwanda cha Sound and Fair ni miongoni mwa shughuli zilizofanyika katika kusindikiza maadhimisho wiki ya Mazingira duniani ngazi ya Mkoa, Mkoa wa Lindi ambayo yamefanyika katika kijiji cha nanjirinji.
Kilwa Masoko
Anuani ya Posta: 160
Simu: 0672365354
Simu: 0672581557
Barua pepe: ded@kilwadc.go.tz /ictsupport@kilwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa