Bonanza la michezo kwa wasichana limefanyika kwa mafanikio makubwa tarehe 09 Mei 2025 katika uwanja wa Chuo cha Maendeleo ya Wananchi (FDC) Kilwa Masoko. Lengo la bonanza hilo lilikuwa ni kuhamasisha ushiriki wa wasichana katika michezo, kuibua vipaji, na kuendeleza afya na mshikamano miongoni mwao.
Timu zilizoshiriki katika bonanza hilo ni:
Kilwa Princess
FDC Queens
Kivinje Secondary Queens
Kilwa Secondary Queens
Katika mashindano hayo, Kilwa Princess wameibuka washindi wa jumla wakifuatiwa na Kivinje Secondary Queens walioshika nafasi ya pili. Ushindani ulioonyeshwa na timu zote umeashiria maendeleo chanya ya michezo kwa wasichana katika Wilaya ya Kilwa.
Afisa Utamaduni, Sanaa na Michezo wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa, Bi. Veneranda Maro, ameeleza pongezi zake kwa wachezaji na waandaaji wa bonanza hilo, akisisitiza umuhimu wa kuendeleza jitihada za kuwawezesha wasichana kushiriki kikamilifu katika michezo kama sehemu ya maendeleo ya jamii.
Tukio hili limekuwa chachu ya kuimarika kwa vipaji vya michezo miongoni mwa wasichana na limeonesha dhamira ya wilaya katika kuwekeza kwenye michezo jumuishi na endelevu
Kilwa Masoko
Anuani ya Posta: 160
Simu: 0672365354
Simu: 0672581557
Barua pepe: ded@kilwadc.go.tz /ictsupport@kilwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa