Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa (Kilwa DC) wameendelea kung’ara katika mashindano ya Shirikisho la Michezo ya Serikali za Mitaa Tanzania (SHIMISEMITA) baada ya kuibuka washindi katika michezo ya kurusha tufe na mkuki. Mashindano haya yamefanyika mkoani Tanga kuanzia tarehe 15 Agosti 2025 na kufikia kilele chake tarehe 29 Agosti 2025.
Mshindi Keneth Hokororo ameibuka shujaa wa Kilwa DC baada ya kutwaa medali mbili za shaba katika michezo hiyo, huku akionesha uwezo mkubwa katika mashindano.
Ushindi huu umeiweka Halmashauri ya Kilwa kwenye ramani ya michezo ya kitaifa, ukionyesha kuwa mbali na majukumu yao ya kila siku ya kiutendaji, watumishi wa serikali za mitaa wana uwezo wa kushiriki kikamilifu kwenye michezo na sanaa, na kufanikisha matokeo yenye heshima kwa taasisi na jamii kwa ujumla.
Aidha, mafanikio haya yanatarajiwa kuwa kichocheo cha kuimarisha mshikamano, kuendeleza ushindani chanya na kuongeza mshikikano wa kijamii miongoni mwa watumishi wa umma nchini.
Kilwa Masoko
Anuani ya Posta: 160
Simu: 0672365354
Simu: 0672581557
Barua pepe: ded@kilwadc.go.tz /ictsupport@kilwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa