Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa imepokea kiasi cha Shilingi 129,297,000.00/= kwa ajili ya kuhaurishwa kwa kaya 4,024 zilizo chini ya mpango wa kunusuru kaya maskini (TASAF). Malipo haya ni kwa ajili ya Dirisha la Malipo la kipindi cha mwezi March – April, 2025 yanatekelezwa katika vijiji vyote vya kilwa ambapo kuna vijiji 90 na mitaa 10.
Zoezi la Malipo linaendelea kuanzia tarehe 03/07 hadi 10/07/2025 ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya zenye uhitaji mkubwa katika Jamii kwa lengo la kuinua hali zao za maisha na kuongeza ushiriki wao katika shughuli za kiuchumi.
Mpango huu ni uthibitisho wa dhamira ya Serikali kuendelea kuimarisha ustawi wa wananchi kupitia usaidizi wa moja kwa moja kwa kaya Maskini.
Kilwa Masoko
Anuani ya Posta: 160
Simu: 0672365354
Simu: 0672581557
Barua pepe: ded@kilwadc.go.tz /ictsupport@kilwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa