Kilwa,
Katibu tawala mkoa wa lindi Bw. Ramadhani Kaswa amewataka viongozi na wanakamati kuhakikisha ujenzi wa majengo katika kituo cha afya masoko unakamilika katika muda uliopangwa.
Ameyasema hayo alipokua wilayani Kilwa katika ziara ya kukagua miradi mbalimbali ambayo inatekelezwa wilayani hapo.
Bw. Kaswa amewataka viongozi na wanakamati kuhakikisha majengo hayo yanakamilika katika muda uliopangwa ili yaanze kutumika kwa kutoa huduma iliokusudiwa kwa jamii ya watu wa Kilwa na viunga vyake.
Katibu tawala mkoa wa Lindi Bw. Ramadhani Kaswa wa pili kutoka kulia akikagua Bati ambazo zinatumika katika ujenzi katika Kituo cha Afya Masoko
Majengo ambayo yanajengwa kituoni hapo ni pamoja na Nyumba ya mtumishi, chumba cha kuhifadhia maiti, mfumo wa uvunaji maji ya mvua, kichomea taka na mengineyo huku fedha zitakazo baki zitatumika katika ukarabati wa baadhi ya maeneo hospitalini hapo.
Ujenzi huo ni utekelezwaji wa dhamira ya dhati ya Mheshimiwa Rais Dk.John Pombe Magufuli ya kusogeza na kutoa huduma bora za afya kwa wananchi.
Akiwa wilayani Kilwa Bw. Kaswa alitembelea miradi mbalimbali ya kimaendeleo ikiwemo mradi wa uoteshaji wa miche ya mikorosho ya kisasa, mradi ambao unasimamiwa na halmashauri ya wilaya ya Kilwa pamoja na kufanya mazungumzo na watumishi na wadau mbalimbali.
Mkurugenzi mtendaji Halmashauri ya wilaya ya Kilwa Bw. Zablon I. Bugingo (kulia) akitoa maelezo kwa juu ya mradi wa uoteshaji wa miche ya mikorosho ya kisasa, mradi ambao unasimamiwa na halmashauri ya wilaya ya Kilwa.
Kilwa Masoko
Anuani ya Posta: 160
Simu: 0672365354
Simu: 0672581557
Barua pepe: ded@kilwadc.go.tz /ictsupport@kilwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa