Kamati ya Siasa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kilwa, ikiongozwa na Mwenyekiti wake Ndg. Said Timamy imeafanya ziara ya kutembelea na kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika Wilaya ya Kilwa leo tarehe 24/02/2025. Ziara hii ni sehemu ya ufuatiliaji wa utekelezaji wa ilani ya Chama cha Mapinduzi ya Mwaka 2020.
Miradi iliyotembelewa katika ziara hii ni ujenzi wa zahanati ya Kijiji cha Miguruwe wenye thamani ya Tsh. 50,000,000/= ikiwa ni fedha kutoka Serikali Kuu, ujenzi wa zahanati ya kijiji cha Njinjo wenye thamani Tsh. 52,000,000/= fedha kutoka mapato ya ndani ya halmashauri na mradi wa ukarabati wa vyumba 6 vya madarasa katika shule ya msingi Kipindimbi wenye Thamani ya Tsh. 100,000,000/= fedha kutoka mapato ya ndani ya Halmashauri.
Akizungumza wakati wa ziara hiyo Mwenyekiti wa kamati ya Siasa Wilaya ya Kilwa Ndg. Said Timamy ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa kwa kusimamia miradi hiyo kwa ufanisi, huku akibainisha kuwa thamani ya fedha inaoenekana na miradi inatekelezwa kwa ubora na viwango vinayostahili.
Akitoa taarifa ya maendeleo ya miradi hiyo Mkuu wa Wilaya ya Kilwa Mhe. Mohamed Nyundo ametoa shukrani zake kwa Kamati ya Siasa ya Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Kilwa, kwa mwongozo na usimamizi mathubuti. Aidha Mhe. Nyundo ameomba kudumisha mshikamano huo katika kuhakikisha maendeleo ya wananchi wa Kilwa yanapatikana kwa kasi Zaidi.
Kilwa Masoko
Anuani ya Posta: 160
Simu: 0672365354
Simu: 0672581557
Barua pepe: ded@kilwadc.go.tz /ictsupport@kilwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa