Kamati ya Siasa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Lindi ikiongozwa na Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Mkoa, Mhe. Kuruthum Issa, imefanya ziara ya kutembelea miradi ya maendeleo kwa lengo la kukagua utekelezaji wa Ilani ya Chama hicho Wilayani Kilwa, Ziara imefanyika Mei 7, 2025.
Ziara hiyo imetembelea miradi yenye jumla ya thamani ya TSh. 44,551,077,124.12 ambayo ni: Mradi wa maji kwa miji 28 wenye thamani ya TSh. 44,007,870,224.12/=, Mradi wa ujenzi wa Nyumba ya mtumishi katika Shule ya Sekondari Mavuji wenye thamani ya TSh. 95,000,000/= na Mradi wa ujenzi wa madarasa 2 katika Shule ya Msingi Naipuli wenye thamani ya TSh 64,000,000/=
Pia kamati imetembelea mradi wa ujenzi wa jengo la Vijana Rika katika Kituo cha Afya Tingi wenye thamani ya TSh 22,006,900/= Pamoja na mradi wa ujenzi wa mabweni 2, madarasa 4 na vyoo katika Shule ya Sekondari Mtanga wenye thamani ya TSh 362,200,000/=
Mhe. Kuruthum kwa niaba ya wajumbe wa Kamati hiyo ametoa salamu za pongezi kwa Uongozi wa Wilaya, Halmashauri na Baraza la Madiwani kwa usimamizi bora wa miradi na utekelezaji mzuri wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi. Aidha, amesisitiza kuendeleza ushirikiano na kuchapa kazi ili kuunga mkono juhudi za Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania za kuleta maendeleo Wilayani Kilwa.
Kilwa Masoko
Anuani ya Posta: 160
Simu: 0672365354
Simu: 0672581557
Barua pepe: ded@kilwadc.go.tz /ictsupport@kilwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa