Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango ikiongozwa Mwenyekiti wa halmashauri Kilwa Mhe. Farida Kikoleka (Diwani wa Kata ya Miguruwe) Imetembelea Miradi ya maendeleo katika Kata ya Kivinje/singino Pamoja na Kata ya Masoko ili kuona kasi ya Ujenzi wa Miradi katika Kata Hizo. Ziara hiyo imefanywa Tarehe 22/04/2025, ambapo kamati imetembelea miradi mbalimbali ikiwemo Mradi wa Ujenzi wa Madarasa mawili yanayojengwa kwa Fedha za Mapato ya ndani Tsh 48,000,000/= katika shule ya msingi Matandu.
Pia kamati imetembelea mradi wa Ujenzi wa Mabweni 2, Madarasa 4 na Matundu ya Vyoo 6 katika Shule ya Sekondari Mtanga wenye Thamani ya Tsh. 362,000,000/= Fedha kutoka Serikali Kuu, Mradi wa ujenzi wa vyumba vya madarasa 2 na Matundu 6 ya vyoo katika Shule ya Msingi Ukombozi wenye thamani ya Tsh. 83,000,000/= Fedha kutoka Serikali kuu.
Sambamba na hiyo Kamati imekagua mradi wa ujenzi wa (vyumba 4 vya madarasa na matundu 2 ya vyoo) wa Shule mpya ya Msingi katika eneo la Mihina wenye thamani ya Tsh 100,000,000/= Fedha kutoka mapato ya Ndani ya Halmashauri.
Wajumbe wameridhishwa na kasi iliyopo katika utekelezaji wa miradi na hali ya usimamizi wa miradi lakini pia wamesisitiza jambo la kuwaisha vifaa vyote vitakavyohitajika vinafika eneo la Mradi kwa wakati ili kuepukana changamoto zinazoweza kujitikeza kipindi hiki cha Mvua.
Kilwa Masoko
Anuani ya Posta: 160
Simu: 0672365354
Simu: 0672581557
Barua pepe: ded@kilwadc.go.tz /ictsupport@kilwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa