Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango ya Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa ikiongozwa na Mwenyekiti wake Mhe. Farida Kikoleka Diwani wa Kata ya Miguruwe,
Imefanya ziara siku tarehe 28/10/2024 ya kukagua na kutembelea miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa kwa Robo ya Kwanza ya mwaka 2024/2025.
Katika ziara hiyo kamati imetembelea mradi wa ukamilishaji wa jengo la zahanati ya Kijiji cha Liwiti kilichopo kata ya Likawage wenye thamani ya TSh. 69,709,800/= ambapo kati ya pesa hizo Tsh 50,000,000/= ni pesa toka Serikali Kuu na Tsh. 19,709,800 ni pesa toka Halmashauri ya Kijiji pamoja na nguvu za wananchi.
Akiongea mbele ya Kamati hiyo, Msimamizi wa mradi huo Ndg. Anderson G. Masanja ambaye pia ni Mtendaji wa Kijiji cha Liwiti ameomba kamati kuuongezea fedha mradi huo ili uweze kukamilika na kuanza kutoa huduma za afya kwa wananchi.
Naye Mhe. Kikoleka ametoa pongezi kwa kamati ya ujenzi wa zahanati hiyo kwa kusimamia vyema matumini ya Pesa za Serikali.
Pia amemuagiza Mhandisi wa Halmshauri kufanya tathmini ya mahitaji yaliyosalia ili kamati iweze kujadili na kufanya maamuzi juu ya ukamilishaji na kuanza kutoa huduma kwa wananchi
Kilwa Masoko
Anuani ya Posta: 160
Simu: 0672365354
Simu: 0672581557
Barua pepe: ded@kilwadc.go.tz /ictsupport@kilwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa