Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango ikiongozwa na Makamu Mwenyekiti wa halmashauri Mhe. Rashidi Msaka (Diwani wa Kata ya Likawage) imeendelea na ziara yake ya kutembelea miradi ya maendeleo siku ya pili katika Kata ya Kipatimu, Mingumbi, Tingi na Somaga tarehe 24/01/2025.
Katika ziara hiyo kamati imetembelea miradi mbalimbali ikiwemo mradi wa ujenzi wa Shule Mpya ya Sekondari katika kijiji cha Mtondo Kimwaga katika kata ya Kipatimu wenye thamani ya TSh.560,552,827/= fedha kutoka Serikali Kuu kupitia mradi wa SRQUIP, ujenzi wa darasa Moja katika Shule ya msingi Naipuli iliyoko katika Kata ya Mingumbi wenye thamani ya Tsh. 23,114,579.76/=
Pia kamati imetembelea mradi wa umaliziaji wa vyumba vitatu vya madarasa katika Shule ya Sekondari Somanga wenye thamani ya TSh. 44,290,440.16/= fedha kutoka Mapato ya ndani ya ndani ya Halmashauri na ujenzi wa madarasa mawili katika Shule ya msingi Mtandago wenye thamani ya TSh.40,000,000/= fedha kutoka Mapato ya Ndani ya ndani ya Halmashauri.
Wajumbe wameridhishwa na kasi iliyopo katika utekelezaji wa miradi na hali ya usimamizi wa miradi lakini pia wamesitiza jambo la kuhakikisha vifaa vyote vitakavyohitajika vinafika eneo la mradi kwa wakati ili kuepukana changamoto zinzaoweza kujitikeza kipindi cha Mvua.
Kilwa Masoko
Anuani ya Posta: 160
Simu: 0672365354
Simu: 0672581557
Barua pepe: ded@kilwadc.go.tz /ictsupport@kilwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa