Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango ikiongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa Mhe. Farida Mohamed Kikoleka, imetoa pongezi kwa Timu ya Menejimenti ya Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa kwa Kuandaa mpango wa kuanzisha Ranchi ndogo katika kata na vijiji vilivyotenga maeneo ya malisho ya mifugo katika mpango wa matumizi bora ya ardhi. Pongezi hizo zimetolewa wakati wa kikao cha Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango kilichofanyika katika Ukumbi wa Chuo cha Maendeleo ya Wananchi (FDC) Kilwa tarehe 21/02/2025.
Akizungumza wakati wa kikao hicho Mhe. Kikoleka amewataka wataalamu kuhakikisha wanawashirikisha wananchi na kuwapatia elimu ya kutosha juu ya utekelezaji wa mpango huo. “Hatutamani kuona ranchi hizi zinamilikiwa na wajanja wachache, hivyo ni lazima jitihada zifanyike kuhakikisha wananchi wanapata elimu na uelewa wa kutosha juu ya mpango huu mzuri ili uweze kuwa na manufaa kwa wengi”.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa Ndg. Hemed Said Magaro ameeleza kuwa Timu ya wataalamu imejipanga vyema kuhakikisha inatoa elimu na hamasa kwa wananchi ili waweze kuelewa lengo la uanzishaji wa ranchi ndogo katika maeneo yao. Hatua hizo ni juhudi za Halmashauri za kuleta suruhisho la migororo baina ya wakulima na wafugaji Wilayani Kilwa.
Kilwa Masoko
Anuani ya Posta: 160
Simu: 0672365354
Simu: 0672581557
Barua pepe: ded@kilwadc.go.tz /ictsupport@kilwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa