Kamati ya Fedha Uongozi na Mipango ikiongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa Mhe.Farida Kikoleka imeridhishwa na taarifa za utekelezaji wa shughuli za maendeleo za Idara na Vitengo kwa kipindi cha Robo ya Tatu (Januari - Machi) cha Mwaka wa Fedha 2024/2025.Kikao hicho kimefanyika Tarehe 24/04/2025 katika Ukumbi wa chuo cha Maendeleo ya Wananchi (FDC) Kilwa
Akizungumza wakati wa kikao hicho Mhe. Kikoleka amemsihi Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa kuendelea kushirikiana na Wataalamu katika kuhakikisha ukamilishaji wa Miradi ya maendeleo kwa wakati ili yalete manufaa kwa wananchi wa Kilwa.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa Ndg. Hemed Said Magaro ameeleza kuwa Timu ya wataalamu imejipanga vyema kuhakikisha utekelezaji wa miradi na shughuli zote zilizopangwa kutekelezwa kwa mwaka wa Fedha 2024/2025 zinatekelezwa kwa wakati.
Kikao hicho ni moja ya Juhudi za kuhakikisha kuongezeka kwa Maendeleo ya jamii ya Kilwa na taifa kwa ujumla.
Kilwa Masoko
Anuani ya Posta: 160
Simu: 0672365354
Simu: 0672581557
Barua pepe: ded@kilwadc.go.tz /ictsupport@kilwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa