Kamati Tendaji ya TEHAMA (ICT STEERING COMMITTEE) Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa imefanya kikao cha robo ya kwanza ya mwaka 2024/2025. Katika kikao hicho taarifa ya utekelezaji wa shughuli za kitengo cha TEHAMA kwa robo ya kwanza ya mwaka 2024/2025 imewasilishwa. Kikao hicho kimefanyika katika ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa leo tarehe 01 Novemba 2024.
Pamoja na kufanya majadiliano juu ya shughuli zinazotekelezwa na kitengo cha TEHAMA, kamati imejadili juu ya maboresho yanayohitajika katika utoaji wa huduma kwa jamii kupitia mifumo ya kidigitali ya TEHAMA, kuhakikisha Usalama wa taarifa za umma kupitia hatua za kiusalama na sera zinazolinda data ndani ya mifumo ya TEHAMA na pia kuboresha ufanisi na uwajibikaji ndani ya Halmashauri kwa kutumia njia za kidigitali za utunzaji wa kumbukumbu na upatikanaji wa taarifa kwa haraka.
Naye mwenyekiti wa Kamati hiyo Ndg. Hemed S. Magaro amesisitiza ufungaji wa mfumo wa GoTHOMIS katika vituo vyote vya kutolea huduma za Afya ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa, Aidha amesisitiza kuweka utaratibu wa kusimika miundombinu ya TEHAMA katika miradi yote inatekelezwa ndani ya Halmashauri kwani karne tuliyopo ni karne ya kidigitali hivyo ni lazima kuzingatia ufungaji wa miundombinu hiyo kwenye miradi hiyo. Pia Ndg. Magaro ameagiza ufungaji wa Kamera za kiusalama katika Hospitali ya Wilaya Kinyonga na Katika Majengo ya Halmashauri.
Kwa Upande Wake Mkuu wa Kitengo cha TEHAMA Ndg. Boniface Kimaro ameileza kamati juu ya mipango iliyopo ya kuhakikisha usimikaji wa Mfumo wa GoTHOMIS katika vituo vyote vya kutolea huduma za afya ndani ya Halmashauri. Pia ameelezea kuwa kitengo kipo katika mchakato wa kuondoa matumizi ya makabrasha katika vikao na kuhamia katika matumizi ya mfumo wa kidigital wa kuendesha vikao yaani e-Board ndani ya Halmashauri.
Kilwa Masoko
Anuani ya Posta: 160
Simu: 0672365354
Simu: 0672581557
Barua pepe: ded@kilwadc.go.tz /ictsupport@kilwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa