Kilwa,
Mkuu wa wilaya ya Kilwa,Christopher Ngubiagai amewataka wakuu wa idara za elimu ya msingi za halmashauri za wilaya ya Kilwa wajitathimini kama wanastahili kubaki kwenye nafasi hizo kama wataweza kuenda na kasi ya utendaji wa serikali ya awamu ya tano.
Ngubiagai ametoa angalizo hilo alipozungumza na wananchi kwenye mkutano wa hadhara katika kijiji cha Mikoma baada ya kukagua ujenzi wa shule shikizi(satelite) katika vijiji vya Pande Ploti na Mikoma Nakimwela
Mkuu huyo wa wilaya licha ya kukiri kwamba kunauhaba wawatumishi, wataalamu na fedha lakini alisema nijambo lisilokubalika kuona ujenzi wa shule shikizi ya kitongoji hicho cha Mpotola umefikia hatua ya kupauwa lakini hakuna ofisa wa idara ya ujenzi wala elimu aliyekwenda kutoa maelekezo na mwongozo kwa ajili ya ujenzi huo.
Ngubiagai alisema licha ya kushindwa kusimamia ujenzi wa shule shikizi lakini pia ujenzi wa vyumba vya viwili vya madarasa ya shule ya msingi Muungano umekwama wakati fedha zipo lakini kumekuwa na urasimu wa kuidhinisha zitumike. Huku wakuu hao waidara wakishindwa kuwapa miongozo walimu jinsi ya kufanya ili wapewe fedha hizo.
Alisema nijambo la kusikitisha kuona wananchi wametumia nguvu zao kujenga jengo la shule lakini wataalamu wa halmashauri wakishindwa kusimamia.Hali inayosababisha jengo hilo kujengwa chini ya kiwango. Kwaupande mwingine baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi Muungano wakisoma chini ya miti wakati fedha zipo lakini kumekuwa na urasimu katika kutoa zitumike.
"Walimu wanazungushwa tu wapofuatilia fedha hizo.Vikwazo na urasimu ni mwingi.Watoto wanasoma chini ya miti,fedha zipo wanawezaje kusoma na kufaulu katika mazingira kama aya.Wananchi watatuelewaje ndugu zangu hii haikubaliki," alisema kwa masikitiko Nubiagai.
Alisisitiza kwamba wakuu wa idara wanasimamia idara zao tu.Hali ambayo nitofauti na wakuu wa mikoa,wilaya na wakurugenzi.Hatahivyo inashangaza kuona wanashindwa kumudu kusimamia kikamilifu yaliyomo kwenye idara zao.Lakiniwanaobeba lawama kutokana na uzembe wao ni wakurugenzi,wakuu wa wilaya na mikoa.
Alisema kutokana na hali hiyo kwanafasi yake hatakubali kubeba lawama yeye wala mkuu wa mkoa kwasababu ya uzembe wao.Hivyo atakabiliana na watendaji wote wazembe.Huku akiweka wazi bora aonekane kuwa ni katili kuliko kuonekana dhaifu aliyeshindwa kuitendea haki nafasi yake kwakushindwa kuwasaidia wananchi.
Wananchi walijitokeza kwenye mkutano wa hadhara katika kijiji cha Mikoma
Kufuatia hali hiyo Ngubiagai aliwataka wakuu hao wa idara wajitathimini kama bado wanaona wanasitahili kubaki kwenye nyazifa zao na wanaweza kumudu kufanya kazi kwa kasi ya utendaji wa serikali ya awamu ya tano.Kwani wakibaini hawawezi waachie ngazi.
Alisema kukosekana kwa usimamizi makini katika miradi inayoibuliwa na kutekelezwa kupitia nguvu na michango ya jamii kunawakatisha tamaa wananchi ambao wameamua kusaidia juhudi za serikali katika kuwapelekea maendeleo.
Mbali na kuwataka wajitathimini,mkuu huyo wa wilaya ya Kilwa amewapa miezi mitatu wakuu hao waidara kwakushirikiana na wananchi wa kijiji cha Mikoma Nakimwera wakamilishe ujenzi wa vyumba vya madarasa.Huku akiwaonya wasikatae kuidhinisha shule shinikizi ya kitongoji cha Mpotola.
"Kesho watakuja hapa watasema shule imejengwa chini ya kiwango haifai.Siwezi kuwaelewa,ikitokea hivyo basi wao ndio wagharamie ujenzi wa jengo jingine nasio wananchi tena,"alionya Ngubigai.
Aidha amempa muda wa mwezi mmoja mhandisi wa ujenzi aandae mpango wa ukamilishaji wa ujenzi wa vyumba hivyo vya madarasa.Huku akiagiza kamati ya ujenzi wa vyumba hivyo vya madarasa kwa kushirikiana na kamati ya shule,idara ya ujenzi na kitengo cha manunuzi wapelekee taarifa za ujenzi wa madarasa hayo kila wiki.
Mbali nakutoa angalizo na maagizo kwa wakuu wa idara na vitengo,Ngubiagai alitoa wito kwa madiwani wa halmashauri ya wilaya hiyo wasaidie kuwabana wakuu wa idara watekeleze na kutimiza majukumu yao kikamilifu.Badala ya kumuachia yeye na mkurugenzi mtendaji.Huku akionya waache kufanyanao urafiki unaopitiliza nakuwa wenye mashaka.
Nae ofisa mipango wa halmashauri ya wilaya hiyo,Kasuka John akijibu malalamiko ya wananchi na kupokea maagizo ya mkuu wawilaya, alisema wanatambua kwamba wananchi kwa kushirikiana na watendaji na viongozi wanawajibu wa kutekeleza miradi ya maendeleo.Hata hivyo taratibu na sheria za manunuzi nilazima zizingatiwe ili kuepuka hoja za ukaguzi.Hivyo wanapohimiza taratibu zifuatwe hawana nia ya kukwamisha miradi au kuwasumbua wahusika.
Kwaupande wao kaimu mkuu wa idara ya elimu shule ya msingi,Mwanaiba Mwichande na kaimu mhandisi wa ujenzi,Yahaya Kapunya walihaidi kutekeleza maagizo ya mkuu huyo wa wilaya kwakusimamia kikamilifu ujenzi wa shule shikizi na kutoa miongozo na ushauri katika kuhakikisha ujenzi wa madarasa unakamilika kwa muda uliopangwa.
_________________________________Mwisho__________________________________________
Credit: Muungwana Blog
Kilwa Masoko
Anuani ya Posta: 160
Simu: 0672365354
Simu: 0672581557
Barua pepe: ded@kilwadc.go.tz /ictsupport@kilwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa