Jeshi la Magereza Wilayani Kilwa likiongozwa na Mkuu wa gereza Kilwa SSP Silverster Hwago limeadhimisha Miaka 64 ya Jeshi la Magereza kwa kufanya zoezi la usafi katika maeneo ya baharini kwa lengo la kutunza mazingira.
Zoezi hilo limefanyika tarehe 23 Agosti 2025 katika eneo la Jimbiza, kando ya Bahari ya Hindi, ambapo Jeshi la Magereza limeungana na makundi mbalimbali ya kijamii yakiwemo vikundi vya jogging. Ushirikiano huo umelenga kuimarisha mshikamano kati ya jeshi na wananchi katika kulinda afya na mazingira.
Akizungumza wakati wa zoezi hilo, (SSP)Hwago amewashukuru wananchi na vikundi vilivyoshiriki, ambapo ameeleza kuwa mshikamano wa kijamii ni nguzo muhimu ya kulinda na kuendeleza maendeleo ya Taifa, na hii inaonyesha mshikamano kati ya wananchi na Jeshi la Magereza katika kuendeleza masuala ya kijamii na mazingira.
Kwa upande wake, Afisa Mazingira wa Wilaya ya Kilwa Boniface achiula amesisitiza umuhimu wa kuendelea kutunza mazingira ya baharini kwa kuwa ni urithi wa kizazi cha sasa na kijacho. Amesema kuwa ushiriki wa taasisi na wananchi katika shughuli za usafi ni chachu ya kujenga jamii yenye afya na mazingira bora.
Aidha, maadhimisho ya mwaka huu yamebeba kauli mbiu isemayo: “Ushirikiano wa Jeshi la Magereza na Jamii kwa Urekebishaji wenye Tija.” Kauli mbiu hii imesisitiza umuhimu wa ushirikiano endelevu kati ya jeshi na wananchi ili kuimarisha heshima, mshikamano na maendeleo ya kijamii.
Kwa pamoja, wananchi na Jeshi la Magereza wamehamasishwa kuendeleza mshikamano huu ili kulinda mazingira, kudumisha afya na kuimarisha maendeleo ya kijamii yenye tija kwa Taifa.
Kilwa Masoko
Anuani ya Posta: 160
Simu: 0672365354
Simu: 0672581557
Barua pepe: ded@kilwadc.go.tz /ictsupport@kilwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa