Idara ya Maendeleo ya Jamii katika Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa Tarehe 28 Machi, 2025 imetoa msaada wa televisheni kwa wafungwa na mahabusu katika gereza la Kilwa Masoko. Msaada huo ulikabidhiwa rasmi kwa Mkuu wa Gereza Kilwa (SSP) Silverster G. Hwago, ambaye alipokea televisheni hiyo kwa niaba ya gereza hilo.
Katika hafla ya makabidhiano, SSP Hwago ameshukuru Idara ya Maendeleo ya Jamii kwa kuguswa na changamoto zinazowakabili wafungwa na mahabusu. Amesisitiza kuwa msaada huo utasaidia kuboresha upatikanaji wa taarifa na burudani, na kuhamasisha mabadiliko chanya miongoni mwao.
"Nichukue fursa hii kutoa Shukrani kwa Wema na Moyo wenu wa kujitoa kwaajiri ya gereza Kilwa mlichokileta ni kikubwa sana kwetu Mungu awabariki"alisema SSP Hwago
Aidha, ametoa wito kwa wadau wengine wa jamii kuiga mfano huo kwa kushiriki katika kusaidia makundi yaliyo katika mazingira magumu. Pia, amebainisha kuwa kuna fursa mbalimbali za mafunzo ya stadi za maisha ndani ya gereza, ambazo jamii inaweza kwenda kujifunza na kuweza kuzitumia kwa maendeleo endelevu.
Idara ya Maendeleo ya Jamii inaendelea
Kushirikiana na taasisi mbalimbali ili kuboresha ustawi wa jamii kwa ujumla.
Kilwa Masoko
Anuani ya Posta: 160
Simu: 0672365354
Simu: 0672581557
Barua pepe: ded@kilwadc.go.tz /ictsupport@kilwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa