Ikiwa ni siku ya sita tangu yalipojitokeza mafuriko katika Wilaya ya Kilwa , idadi ya waathirika imeendelea kuongezeka kutoka elfu nne mpaka kufikia Zaidi ya watu elfu tisa wanaishi katika kambi mbali mbalia za kuwahudumia wahanga wa mafuriko.
Mpaka sasa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya pamoja na ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji imepokea misaada mbali mbali ya kijamii ambapo mpaka leo tarehe 31 Januari shirika la kikristo linalowahudumia wakimbizi la Tanganyika Christian Refugee Service (TCRS) limekabidhi nguo marobota mia tatu kwa ajili ya wahanga wa mafurika.
Misaada hiyo imekabidhiwa kwa Mkuu wa Wilaya Mhe.Christopher Ngubiagai na Afisa Miradi anayesimamia Ushauri na dharura kutoka TCRS Bi.Teddy Deo katika ofisi za Halmashauri ya Wilaya ambapo ameahidi kuendelea kutoa misaada ya kibinadamu ili kuendelea kuwapa
Mkuu wa Wilaya amewapongea wadau hao na kuwaambia kwamba bado mahitaji ni makubwa na hasa ya chakula katika kambi hizo.
Akitaja idadi ya waathirika wanaohudumiwa katika kambi mbali mbali, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa Ndg.Ally Ligalawike amezitaja kambi kumi za kuhifadhi wahanga na idadi ya watu kwenye mabano kama ifuatavyo;
Kituo cha Njinjo watu (6440),Mitole watu (790),Kikole watu (93),Kiranjeranje watu (377),Pamoja naMakangaga watu (589).
Amevitaja vituo vingine vyenye watu kuwa ni,Ruhatwe watu (550),Matandu watu (663),Nakiu watu (126)
,Kigombo watu (134) na Likumla watu (98) na kufanya jumla ya watu wanaohudumiwa kufikia watu 9,860.
Kaimu Mkurugenzi huyo ameendelea kutoa wito kwa wadau mbali mbali kuendelea kutupia macho Wilaya ya Kilwa kwani madhara ni makubwa sana kutokana na miundombinu na makazi ya watu kuathirika kwa kiwango kikubwa ambapo amezitaja changamoto zinazohitaji msaada wa haraka kuwa ni Chakula, Nguo, madawa, maji safi na salama, mahema ya Kuishi pamoja na vyombo vya usafiri kama magari na mafuta kwa ajili ya kuwawezesha kuwafikia wahanga wanaohudumiwa kila siku.