• Malalamiko |
    • Anuani Zetu |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
Kilwa District Council
Kilwa District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Mikakati ya Halmashauri
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Afya
      • Utumishi na Utawala
      • Elimu ya Msingi
      • Mipango na Takwimu
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Ujenzi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Mifugo na Uvuvi
      • Fedha na Biashara
      • Maliasili
    • Vitengo
      • Usafi na Mazingira
      • Sheria
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Uchaguzi
      • Ugavi
      • TEHAMA
      • Nyuki
      • Biashara
      • TASAF
      • Lishe
      • Uvuvi
    • Miji Midogo
      • Masoko
      • Kivinje
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Huduma za Uwekezaji
    • Biashara na Viwanda
    • Madini
    • Uvuvi
    • Utalii
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
    • Mikopo kina Mama na Vijana
    • Huduma za Maji
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Uchumi Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
    • Ratiba ya Vikao vya Kisheria
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Itakayo tekelezwa
  • Machapisho
    • Muongozo
    • Utaratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Picha
    • Habari
    • Matukio
  • Mifumo
    • PlanRep
    • FFARS
    • Prem
    • Salary Slip Portal

Hivi hapa vivutio ishirini na nane vinavyopatikana kilwa

Posted on: November 15th, 2018

 

VIVUTIO VYA UTALII VYA RASIMALI ZA URITHI (CULTURAL AND NATURAL RESOURCES WILAYA YA KILWA

NA.

VIVUTIO

KIVUTIO KILICHOPO NA JINSI YA KUKIFIKIA

                         MAELEZO YA KIVUTIO  
1.
Bandari ya uvuvi ya Masoko
Kutoka Masoko Sokoni kwa kutembea kwa miguu ni mwendo wa dk 15.
Eneo lenye ufuko mkubwa wenye mchanga, watu wa Masoko hukutana na wavuvi.
Eneo lenye shughuli nyingi, mashua hutengenezwa na zingine hukarabatiwa.
2.
Kijiji cha uvuvi cha Makumbuli
Ni Kijiji kidogo cha uvuvi, kwa kutembea kwa miguu kutoka Soko la Masoko ni takribani mwendo wa  dk 15. Ili kufika kwa urahisi ulizia Kanisa la Lutheran, kutoka Kanisani tembea kuelekea Baharini.
Kipo pembezoni mwa msitu wa mikoko.
Hapa hupatikana chakula kwa kitoweo cha Samaki na kaa, usafiri wa mitumbwi hupatikana na ndege wa aina mbalimbali unaweza kuwaona kwenye mikoko.
3.
Ngazi ya Watumwa
Eneo hili lipo Pwani ya kusini ya Masoko, linatazamana na Eneo la Kilwa Kisiwani.  Kutoka Masoko Mjini kwa kutumia baiskeli unatumia dk 10, wakati kwa mguu unatumia dk 25.
Eneo lililohifadhiwa ambalo ukisimama hapo unaweza kuona mimea na viumbe mbalimbali wakiwemo viumbe wa baharini.
4.
Kisiwa cha Rukila
Kisiwa kidogo kilichopo kilomita 12 kutoka bandari ya Masoko… unachukua mwendo wa saa 1:30 kwa boti.  Wakati wa maji kupwa unaweza  kutembea kwa miguu kufika kisiwani kwa kutumia muda wa saa 3 ila unatakiwa uwe na mtu mzoefu vinginevyo unaweza ukazingirwa na maji, wakati wa maji kujaa.
Makazi yenye bayoanuwai kubwa ya samaki na matumbawe.
Uzamiaji  kwa ajili ya kuangalia matumbawe na samaki unafanyika pia unaweza kuangalia ndege na unaweza kulala hapo kama wavuvi wanavyolalala.
5.
Kilwa Kisiwani
Kilwa Kisiwani inafikika kwa kutumia boti.  Kwa  boti yenye injini unatumia dakika 20. Kwa kutumia mashua inapendeza sana ila inatumia muda mrefu kidogo kutegemeana na hali ya hewa.
Kisiwani ni Mji Mkongwe kabisa wenye magofu ya kuanzia karne ya 11 mpaka karne ya 19. Ni eneo ambalo liko kwenye Orodha ya UNESCO ya Urithi wa Dunia tangu mwaka 1981.
Unaweza kutumia siku nzima kutembelea vivuvio vilivyo  Kilwa Kisiwani.  Pia kuna ndege wa aina mbalimbali.
6.
Jiwe la Jahazi
Jiwe /mwamba upo kaskazini Mashariki mwa Kilwa Kisiwani. Eneo hili  linaweza kufikika kwa boti kutoka Masoko au kwa miguu kutoka bandari ya Kilwa Kisiwani.
Inasadikikika hili lilikuwa ni jahazi halisi lililokuwa linatumiwa na maadui waliotaka kuwavamia Wenyeji lakini maombi maalum (Al-badir) yalifanywa yakageuza Jahazi kuwa jiwe.
7.
Songo Mnara
Ipo kilomita 12 kusini mwa Masoko, chini ya Kilwa Kisiwani.  Kwa kutumia boti ya injini unatumia chini ya saa moja.
Kama ilivyo Kilwa Kisiwani eneo la Historia na maarufu kwa utamaduni wa Kiswahili (Swahii Culture). Kuna magofu ya tangu karne ya 15 AD ulikuwa ni Mji wa mawe (Stone town)
8.
Sanje ya kati na Mbuyu  Mbugu.
Kisiwa hiki kipo Mashariki mwa Songo Mnara ni kilomita 14 kutoka bandari ya Masoko. Kwa boti ya injini unatumia dakika 45 na mashua saa 1:30 kama hali ya hewa ni shwari.
Hapa unaweza kufanya safari ya boti kupita Kokoni huku ukiangalia ndege wa kila aina.  Pia wakati unaposafiri unaweza kuona hatua mbalimbali za shughuli za uvuvi kuanzia kuvua mpaka ukaushaji wa samaki kwenye ufuko.
Pia kuna mbuyu mmoja wa kuvutia sana ambao una pango/shimo kubwa. Mchanga mzuri mweupe uliopo ufukoni ni mzuri kwa kuogelea, kupumzika na hata kupiga kambi.
9
Pandawe Malalani
Eneo la Pandawe lipo Kijiji cha Malalani huko Pande.  Ni kilomita 130 kutoka Mjini Masoko na huchukua saa 2:30 kufika Malalani kwa kutumia gari.   Kisha inabidi kutembea kwa dakika 15.
Inasemekana kwamba katika eneo hili mtu mmoja mrefu sana aliyeitwa Unji bin Unuki alizama/didimia kwenye tope na  hii inathibitishwa na mawe ya jiko alilokuwa akitumia na nyayo zake (footprints) zilizopo hapo.
10
Mwanakiwambi
Magofu haya yapo Kusini mwa Songo Mnara.  Unaweza kufika huko kwa kutumia boti kwa saa 2:30 kutokea Masoko au kwa miguu kutokea Songo Mnara kwa saa 4.
Ni eneo la Kihistoria ambalo halijahifadhiwa hadi leo.  Kuna magofu jirani na maji/bahari.
11
Milima ya Matumbi
Milima ya Matumbi ipo Magharibi mwa Kilwa Kijiji Kikuu ni  Kipatimu ambacho kipo juu ya milima hii umbali wa Kilomita 117 kutoka Mjini Masoko.
Eneo hili lina madhari nzuri yenye Vijiji vidogo vidogo, mibuyu, mito na mashamba yaliyopandwa vizuri/kwa uangalifu (migomba, minazi na Mihogo ).  Eneo hili pia kuna mapango mengi.
12
Mapango ya Nandembo
Mapango yapo Kijiji cha Nandembo, Kilomita 8 kutoka Kijiji cha Kipatimu.
Hapa kuna mapango kadhaa unawezs kuyaona.
Inashauriwa usiingie kwenye pango la Nangoma kwani kuna kundi kubwa la popo ambao wanaweza kusababisha madhara.
Nangoma ni pango lililotumiwa kujifichia wakati wa vita ikiwemo vita vya Majimaji .  Pango jingine linaitwa Nangoma namba 2 (Nangoma 2) pango hili unaweza kuingia, pango ambalo pia lina maji.
13
Mapango ya Namahingo
Mapango haya yapo Kijiji cha Namahingo kilomita 12 kutoka Kipatimu.  Unahitaji mwongozaji kwani milango ya mapango haya yamefichwa na msitu mkubwa.
Mapango haya yanavutia sana kwani yana mapito ya asili (Organic Corridors) ambayo yanaelekea kwenye vyumba mbalimbali, mito na kwenye akiba za maji (Water reseivours). Pango hili pia hutumika kama chanzo cha maji kwa binadamu hasa wakati wa Kiangazi.  Baadhi ya mapango haya ni makazi ya makundi makubwa ya popo, hivyo inashauriwa watu wasiingie.
14
Ziwa Maliwe
Ziwa hili lipo kilomita 84 kutoka Masoko kwa gari ni mwendo wa saa 3 kutoka Masoko, unakwenda kilomita 29 hadi Nangurukuru(dk 30),kisha unatumia barabara ya vumbi magharibi kiomita 53 mpaka Kijiji cha Ngea mwendo wa saa 2:30 (Mwongozaji anahitajika )
Ziwa Maliwe ni ziwa nzuri lilotulia na unaweza kutumia mitumbwi ya wavuvi kujionea aina mbalimbali za viumbe. Unaweza pia kuwaona Viboko, Mamba na pia makundi makubwa ya ndege, vyura na wadudu mbalimbalii hasa nyakati za Kiangazi.  Wanyama wengi pia hufika hapo kunywa maji wanyama kama nyani, Tembo na Ngiri.
15
Ngumbi ya Sukani
Eneo hili lipo km 36 Kusini mwa Masoko. Kwa njia ya barabara huchukua saa 2 kufika Kijiji cha Nakimwela.
Ngumbi ya sukani maana yake angalia kwa makini, uwe mwangalifu .  Eneo hili ni hatari sana lina mawimbi makali na mwamba mkubwa (linafahamika sana na Wavuvi)
16
Rasi Ng'umbi
Eneo hili lipo jirani na Lihimalyao umbali wa km 123 kutoka Kilwa Masoko
Rasi yenye mawemawe na mawimbi ya bahaari.  Mawimbi hupiga kwenye mwamba wa Matumbawe na kusababisha matundu matundu.  Unapoelekea kwenye rasi utaona ndege wa aina mbalimbali kama hornbill, njiwa, Tai na wengine.  Ukiwa huko pia unaweza kutembelea Makaburi ya Mkazambo, Msikiti wa Mtumbu, Msitu wa ajabu wa Mtimilu na pia kuna unyayo Mkubwa.
17
Mapango ya Mkurukara
Eneo hili lipo jirani na Lihimalyao umbali wa km 123 kutoka kilwa Masoko
Mkurukara maana yake ni Kiongozi.  Mapango haya yalitumika kama nyumba au sehemu ya kupumzikia kwa kiongozi na wafuasi wake.  Kina mapango mawili moja lilitumika kama nyumba na jingine lilitumika kusambaza maji.  Maji haya yanatumika hadi leo kwa shughuli za matambiko.  Inasadikiwa kuwa maji haya yana nguvu ya uponyaji hivyo yana thamani kubwa kwenye Matambiko.
18
Kisima cha maji cha Mwanalinda
Kisima cha maji cha Mwanalinda na Mapango ya Ngarwe yapo Kusini mwa Lihimalyao unaweza kwenda kwa gari au pikipiki.
Wanavijiji toka Vijiji jirani wanategemea maji kutoka mapango haya maji ambayo yanasadikika kuponya maradhi lakini pia yana nguvu za miujiza ambayo humwondolea mtu mkosi na unapoyaoga.
19
Mapango ya Ngarwe
Kisima cha maji cha Mwanalinda na Mapango ya Ngarwe yapo Kusini mwa Lihimalyao unaweza kwenda kwa gari au pikipiki.
Wanavijiji toka Vijiji jirani wanategemea maji kutoka mapango haya maji ambayo yanasadikika kuponya maradhi lakini yana nguvu za miujiza ambayo humwondolea mtu mkosi na unapoyaoga
20
Pango Tung'ande
Pango ya Tun'gande lipo Kusini mwa Lihimalyao.
Pango hili lina hewa  na mwanga wa kutosha huitaji kwenda na taa.  Ndani ya hili pango kuna sanii mbalimbali za zamani ikiwamo ya Tembo, Kiti cha Mfalme na Jiko. Ukiwa ndani ya pango hili unaweza kutumia zaidi ya masaa 2 kuzunguka.
21
Msikiti wa Mtumbu na unyayo wa Binadamu
Msikiti wa Mtumbu na unyayo wa Binadamu vipo katika Kijiji  cha Ruyaya.  Unaweza kwenda kwa gari au boti  Ruyaya ipo umbali wa kilomita 123 kutoka Masoko Mjini.
Msikiti wa Mtumbu ulijengwa na Waomani karne ya 15, sehemu ya msikiti huu imebomoka.  Wanakijiji pia wanaliona eneo  hili kama ni la tambiko.  Hapa pia kuna unyayo wa mtu mrefu sana (Unji bin Unuki)  aliyeweza kukamata samaki kwenye kina kirefu baharini na kumwoka/kumchoma (grill) samaki huyo kwenye jua.  Mtu huyu pia alijulikana kwa jina Nanganana 'Nangakumbi'.
22
Kiswele
Kiswele ipo kusini mwa Wilaya ya Kilwa, km 120 kutoka Masoko Mjini.
Kijiji cha uvuvi.  Ilikuwa kambi ya Waingereza wakati wa vita ya kwanza ya Dunia ambapo mahali walipohifadhia risasi, pia hapa unaweza kupanda kilima Pandawe ambapo matambiko hufanyika.
23
Rushungi
Ni Kijiji kidogo kilichopo ukanda wa Pwani umbali wa Kilomita 140 kutoka Masoko Mjini. Katika barabara iendayo Lindi nenda Kushoto umbali wa kilomita 5 kutoka Kijiji cha Mandawa.
Wafanyabiashara wa kihindi walijenga ghala kubwa (store house) bandari kwa ajili ya kusafirisha Mkonge hadi bandari ya Tanga . Mashua kubwa zilizotumika kusafirishia mkonge zipo hadi  leo.
24
Bwawa la mto Nyange
Bwawa hili lipo upande wa kusini mwa Wilaya ya Kilwa Kilomita 140 kutoka Masoko Mjini.  Unaweza kufika hapa kwa kutumia gari baada ya hapo utahitaji utembee kwa muda wa  robo saa ili ulifikie hilo bwawa.
Bwawa hili ni kivutio kikubwa ambapo kuna viboko wengi wanaosadikiwa kuwa ukiwaita wanajitokeza kwa wingi.  Wakati mzuri wa kuwaona viboko  hawa ni wakati maji yanapokuwa yamejaa.
25
Mapango ya Kiwawa
Pango kubwa lipo Kijiji Kiwawa, isipokuwa Mapango mengine yanapatikana eneo la Kiukula.  Kutoka Masoko Mjini hadi Kiwawa ni Kilomita 70 ambapo unaweza kutumia saa 1:30 kufika.
Haya ni mapango makubwa yenye hewa na mwanga wa  kutosha ambapo unaweza kutembea bila kuhitaji tochi.
26
Ngurumu Mchakama Mavuji
Ngurumu ipo Mchakama katika Kijiji cha Mavuji.  Unaweza kufika huko kwa gari au pikipiki . Mchakama ipo umbali wa kilomita 65 kutoka Masoko Mjini ni mwendo wa takribani saa 1:30
Ngurumu ni mto unaopita katikati ya miamba miwili (two rock formations) na unatoa maji kwa Wanavijiji wengi. Zipo imani nyingi zinazohusishwa na mto huu.  Mto huu pia unajulikana kwa jina la Mwalimkoto, Mwalimkoto ni jina na Msichana mmoja aliyepotea baada ya kwenda kuchota maji katika huu mto kwani mila hazikuruhusu.
27
Kilwa Kivinje
Ni eneo lilo Kaskazini ya Kilwa Masoko, yako umbali wa takribani Kilometa 30 kutoka Masoko na kilometa takribani 3 kutoka Singino ni mwendo wa takribani nusu saa kutoka Kilwa Masoko.
Historia na kukua kwa Kilwa Kivinje, ni matokeo ya harakati za kibiashara za wayao karne ya 17 na kusambaa kwa dola la washirazi katika ukanda wa Pwani ya Afrika mashariki na kukua kwa biashara ya utumwa mnamo karne ya 18.  Kwa sasa Mji wa Kivinje bado una majengo ya karne 19 ambayo yanapatikana Mtaa wa Mgongeni, yakiwa bado na milango ya Kiswahili.
28
Sanje ya Majoma
Yako katika Kijiji la Songo Mnara, Kusini mwa Magofu ya Songo Mnara Sangarungu.
Inajumuisha mlolongo wa magofu takribani nane, misikiti na makaburi yanayokadiriwa kuwa ya karne ya 13 BK, wakati biashara na maendeleo ya Kilwa yalikuwa ya juu sana.

Matangazo

  • TANGAZO KWA UMMA KUHUSU UTOAJI WA MIKOPO KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU October 04, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI October 11, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI September 27, 2024
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI. April 25, 2023
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • MAKALA APONGEZA JITIHADA ZA KURUDISHA MAWASILIANO SOMANGA

    April 10, 2025
  • Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoa Mkono wa Eid kwa watoto wenye mahitaji Maalum Shule ya Msingi Mtanga Wilayani Kilwa.

    March 31, 2025
  • IDARA YA MAENDELEO YA JAMII YATOA MSAADA WA TELEVISHENI KWA GEREZA LA KILWA MASOKO

    April 28, 2025
  • MARAFIKI WA ELIMU WAWASILISHA TAARIFA YA UFUATILIAJI WA MAKUZI YA AWALI YA MTOTO KWA WADAU WA ELIMU KILWA.

    April 28, 2025
  • Tazama Zote

Video

Mkuu wa Wilaya ya Kilwa Akipokea Mwenge wa Uhuru.
Video Zaidi

Kurasa za Haraka

  • TARURA GPN
  • Watumishi Portal
  • MIKOPO 10%
  • Mikopo ya Wanawake na Vijana
  • Huduma za Elimu

Tovuti Muhimu

  • Utumishi
  • Tamisemi
  • Ikulu
  • Wizara ya Fedha
  • Wizara ya Elimu
  • Lindi

Idadi ya Watembeleaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Watembeleaji

writingMasterThesis

Ramani ya Mahali

Anuani Zetu

    Kilwa Masoko

    Anuani ya Posta: 160

    Simu: 0672365354

    Simu: 0672581557

    Barua pepe: ded@kilwadc.go.tz /ictsupport@kilwadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Kanuni Binafsi
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa