Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa imetoa mikopo kwa vikundi vya vijana, wanawake na walemavu yenye thamani ya Shilingi milioni Mia moja kumi na moja na laki nane ambayo ni asilimia kumi ya makusanyo ya mapato ya ndani hadi kufikia kipindi cha robo ya kwanza ya mwaka 2018/2019.
Utoaji wa mikopo hiyo ni utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya Chama cha mapinduzi ya mwaka 2015 ibara ya 57-61 ambayo inataka kuwawezesha wananchi kiuchumi.
Akizungumza baadfa ya makabidhiano hayo Mkurugenzi mtendaji wa HaImashauri ya Wilaya ya Kilwa Ndg. Renatus Mchau amesema anaamini wanufaika wa mikopo hiyo wataitumia kwa malengo yaliyokusudiwa na hatimae kuleta matokeo chanya.
“Imani yangu wananchi waliofaidika na mkopo huu watautumia ipasavyo ili kujiongezea kipato na kuboresha maisha yao” alisema mchau
Aidha ameahidi kuendelea kutoa mikopo kadri itakavyokusanywa na kuwataka vijana kuunda vikundi vyenye malengo ya kiuchumi ili waweze kufaidika na mikopo hiyo.”
“Tutaendelea kutoa mikopo kadri tutakavyokusanya na niwahimize hasa vijana kuunda vikundi vyenye malengo ya kiuchumi ili tuweze kuwasaidia kupitia fungu hili” alisisitiza Mchau
Kilwa Masoko
Anuani ya Posta: 160
Simu: 0672365354
Simu: 0672581557
Barua pepe: ded@kilwadc.go.tz /ictsupport@kilwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa