Halmashauri ya Wilaya Kilwa imetoa mikopo ya asilimia 10 kiasi cha Tsh. Bilioni 1,361,178,000/= ikiwa ni pamoja na guta 8, Trekta 1, Pikipiki 86 na vifaa vya ujenzi kwa vikundi 283 vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu, juhudi hizi ni sehemu ya mpango wa serikali wa kuinua wanachi wake kiuchumi.
Akikabidhi hundi hiyo Mkuu wa Wilaya ya Kilwa Mhe. Mohamed Nyundo amewataka Maafisa maendeleo ya Jamii Wilayani Kilwa kuwasaidia wananchi kusimamia vyema Miradi waliochagua. Pia amewasisitiza wanachi kutokutumia mikopo hiyo kwa ajili ya shughuli nyingine tofauti na zile walizopanga kutekeleza.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa Ndg. Hemed S. Magaro amewasisitiza wanufaika wa mikopo hiyo kuitumia vizuri mikopo waliyoipata kuongeza kipato, kujiimarisha kiuchumi na kufanya marejesho ya mikopo yao kwa wakati ili itumike kukopeshwa kwa wananchi wengine wenye mahitaji.
Kwa upande wao wanufaika wa mikopo hiyo wameishukuru serikali ya Awamu ya Sita chini ya Uongozi wa Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kukubali kurejesha mikopo isiyo na riba kwa wananchi kwani mikop iyo itaenda kuwa chachu ya maendeleo na kuwaimarisha kiuchumi.
Kilwa Masoko
Anuani ya Posta: 160
Simu: 0672365354
Simu: 0672581557
Barua pepe: ded@kilwadc.go.tz /ictsupport@kilwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa