Shirika la Ushirikiano wa Kimataifa la Ujerumani GIZ, katika kuhakikisha linasaidia Shughuli za Maendeleo endelevu katika jamii, limefanya Kikao na Timu ya Menejimenti ya Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa ili kuwasilisha mpango kazi na mikakati ya shirika hilo juu utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo ndani ya Wilaya ya Kilwa hususani katika mpango wao wa Pwani Yetu Project katika sekta ya Uvuvi. Kikao Hicho Kimefanyika leo tarehe 18/03/2025 Katika Ukumbi wa Sultani Kilwa Masoko
Miongoni mwa Miradi iliyotajwa ni Uendelezeaji wa Ujenzi wa Soko la samaki na ujenzi wa Chanja za Kisasa katika kata ya Somanga ambalo linatarajiwa kusaidia katika Shughuli za uvuvi na kuongeza thamani ya mazao ya Baharini,Pia kuimarisha Mazingira ya uhifadhi na uchakataji wa samaki
Mbali na hayo, GIZ imeeleza mpango wake wa kutoa elimu kwa jamii kuhusu umuhimu wa kulinda Mazingira ya Bahari ili kuhakikisha utunzaji wa rasilimali za Baharini kwa matumizi ya sasa na vizazi vijavyo
Akizungumza katika kikao hicho Meneja wa Mradi kutoka GIZ Ndg. Ralf Senzel amesema mipango hii itaenda kusaidia kuongeza thamani ya Mazao ya bahari kutokana na mazingira bora yatakayo tengenezwa wakati wa utekelezaji kama vile Mazingirza bora ya uchakataji na uhifadhi samaki tofauti na inavyotumika katika jamii hizo.
Ikumbukwe GIZ itatekeleza shughuli hizi za Maendeleo kupitia WWF ambao watafanya usimamizi wa Shughli zote ikiwemo kusimamia Mradi wa Soko la samaki la Somanga, utoaji wa Elimu katika jamii juu ya ulindaji wa Mazingira ya bahari.
Kilwa Masoko
Anuani ya Posta: 160
Simu: 0672365354
Simu: 0672581557
Barua pepe: ded@kilwadc.go.tz /ictsupport@kilwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa