Mkuu wa mkoa wa Lindi Mhe. Godfrey Zambi amewataka wananchi ambao kata zao zinaenda kufanya uchaguzi kuwa watulivu na kujiepusha na vitendo vitakavyo hatarisha amani
Zambi ameyasema hayo alipokuwa akihitimisha ziara ya siku Sita wilayani Kilwa katika viwanja vya Maalim Seif Mjini Kilwa Kivinje Novemba 12 mwaka huu
Zambi amesema akiwa kama Mweneykiti wa kamati ya ulinzi na usalama Mkoa atashughulika na wale wote watakao jihusisha na vitendo vya uvunjifu wa amani kipindi cha uchaguzi pamoja na watakao fanya kampeni za matusi.
Aidha amewataka wananchi kuchagua viongozi kwa kupima Nguvu za hoja na sio hoja za nguvu
Akiwa wilayani Kilwa Mhe. Zambi aliambatana na wataalamu kutoka Halmashauri ya wilaya ya kilwa na kufanya mikutano katika vijiji mbalimbali pamoja na kusikiliza na kuzishughulikia kero za Wananchi.
Kilwa Masoko
Anuani ya Posta: 160
Simu: 0672365354
Simu: 0672581557
Barua pepe: ded@kilwadc.go.tz /ictsupport@kilwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa