Katika Juhudi za kuongeza Maendeleo ya Kiuchumi Wilayani Kilwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Kilwa Ndg. Hemed S. Magaro Akutana na wafanya Biashara wa Hoteli pamoja na Nyumba za kulaza wageni ili kusikiliza changamoto zao.
Aidha amewaomba wafanya Biashara wanaojihusiha na Utalii wa fukwe Wilayani Kilwa kupunguza gharama za upatikanaji wa huduma hiyo ili kuweza kuongeza chachu kwa wenyeji kutembelea katika maeneo hayo jambo ambalo litapelekea kuongeza mapato katika Biashara zao.
Ndg. Magaro ameyaeleza hayo wakati akizungumza na wafanya biashara Wa Hoteli pamoja na Nyumba za kulaza wageni katika ukumbi wa Chuo Cha Maendeleo (FDC) Tarehe 16/01/2025 Kilwa ambapo amesema kuwa watu mbalimbali wanatamani kufanya zaidi Utalii wa ndani, lakini wanashindwa kutokana na Huduma hizo kuzidi vipato vyao.
Aidha Afisa Biashara wa Wilaya ya Kilwa Ndg. Peter Ngoti amewataka wafanya biashara hao kuzingatia ulipaji wa Tozo za Kiserikali ikiwemo Kodi na kulipia Leseni ili waweze kufanya Biashara zao bila kuvunja Shaeria na kanuni za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Kilwa Masoko
Anuani ya Posta: 160
Simu: 0672365354
Simu: 0672581557
Barua pepe: ded@kilwadc.go.tz /ictsupport@kilwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa