Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa Ndg. Hemed S. Magaro amewataka watumishi wa afya wilayani Kilwa kufanya kazi kwa moyo katika kuhudumia wananchi ili kupunguza malalamiko katika vituo vyao. “Najua zahanati zinafungwa saa tisa na nusu lakini ukiitwa nenda ukawahudumie watu”
Hayo yamezungumzwa wakati wa kikaokazi baina ya Mkurugenzi Mtendaji, na Waganga Wafawidhi wa Hospitali, Vituo vya Afya na Zahanati Wilayani Kilwa kilichofanyika katika Ukumbi wa Chuo cha Maendeleo ya Wananchi (FDC) Kilwa, tarehe 12/02/2025.
Aidha Ndg. Magaro amesisitiza matumizi ya mfumo wa GoTHOMIS katika ukusanyaji wa mapato ya serikali ambapo ameeleza kuwa, mapato yakikusanywa kwa ukamilifu yatakuwa chachu ya kutoa huduma bora za afya hivyo kupelekea kufikia malengo yaliyowekwa na serikali ikiwemo kutokomeza malaria na kutoa chanjo kwa idadi kubwa ya watoto.
Sambamba na hayo Ndg. Magaro ametoa pongezi kwa juhudi kubwa wanazofanya katika utoaji wa huduma za Afya, Pia amewataka watumishi hao kutumia lugha nzuri katika kutoa huduma, kujenga hali ya urafiki na wananchi wanaowahudumia, kuboresha na kupendezesha mazingira katika vituo vyao kwa kupanda maua na miti ya kivuli.
Kilwa Masoko
Anuani ya Posta: 160
Simu: 0672365354
Simu: 0672581557
Barua pepe: ded@kilwadc.go.tz /ictsupport@kilwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa