Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya kilwa Ndg.Hemed Magaro amewataka Maafisa Watendaji Ngazi za Kata kuendelea kutekeleza agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kusimamia swala la lishe katika kata na vijiji wanavyofanyia kazi. Hayo ameyasema wakati wa kikao cha Tathmini ya Mkataba wa Lishe Kota ya tatu (Januari -Machi) ya Ngazi ya kata na Vijiji kilichofanyika katika Ukumbi wa Chuo cha maendeleo ya Wananchi (FDC) kilwa tarehe 23/04/2025.
Katika utekelezaji wa hatua hiyo Ndg. Magaro amewaagiza Watendaji hao kuongeza nguvu kwenye utoaji wa elimu ya lishe kwa wataalamu wengine ngazi ya Kata pamoja na waheshimiwa Madiwani na Wenyeviti wa Vijiji ili kuhakikisha wanaelewa umuhimu wa lishe kwa watoto mashuleni na jamii wanayoongoza.
Pia amewaagiza watendaji hao kuhakikisha wanajipanga vizuri kutoa elimu ya lishe kwa wananchi kupitia mikutano au matukio mbalimbali ya kijamii ili kuwahamasisha wazazi kuchangia kiasi cha fedha ili kuwawezesha wanafunzi kupata chakula wawapo mashuleni. “ukienda kanisani sema, ukienda msikitini sema, ukienda kwenye tukio la michezo sema” alisema Ndg. Magaro
Aidha katika kuitimisha kikao iko Ndg. Magaro amewapongeza wajumbe wa kamati ya lishe wilaya kwa kuongeza Idadi kubwa ya shule zinazotoa chakura shuleni hatua hiyo imesaidia katika kuongeza kiwango cha Ufaulu kwa Kiasi Kikubwa katika Wilaya ya Kilwa.
Kilwa Masoko
Anuani ya Posta: 160
Simu: 0672365354
Simu: 0672581557
Barua pepe: ded@kilwadc.go.tz /ictsupport@kilwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa