Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya kilwa Ndg. Hemed Said Magaro amewataka wataalamu wa lishe Wilayani Kilwa kuyatumia makundi ya watu wenye ushawishi katika jamii kama Wazee Maarufu, Viongozi wa Dini, Viongozi wa Vyama vya Siasa na Viongozi wa Kimila ili kuhamasisha wazazi juu ya umuhimu wa uwepo wa chakula kwa wanafunzi wawapo mashuleni.
Hayo yameelezwa wakati wa kikao cha Kamati ya Lishe ya Wilaya ya Kilwa kilichofanyika kwa lengo la kujadili utekelezaji wa Idara na Vitengo kwa Kipindi cha Oktoba – Desemba 2024 katika Ukumbi wa Chuo cha Maendeleo ya Wananchi (FDC) Kilwa tarehe 12/02/2025.
Aidha, Ndg. Magaro amewataka wataalamu kuweka mikakati ya Kiidara ya kuhakikisha wanaanzisha utaratibu wa mikutano shuleni kwa ajili ya kuhamasisha na kuwashawishi wazazi kuchangia chakula shuleni. “Sio lazima watoto waanze na ugali au wali, wakipata hata uji inatosha, wazazi wasiambiwe vitu vingi kwa wakati mmoja, waanze taratibu taratibu baadae watazoea na wataweka mambo sawa” Amesema Ndg. Magaro.
Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Wilaya ya Kilwa Ndg. Fredrick Moshi amewasisitiza wajumbe wa kamati hiyo, kuhakikisha wanatenga kiasi cha fedha katika bajeti za Idara na Vitengo vyao kwa ajili ya utekelezaji wa hafua za lishe Wilayani Kilwa.
Kilwa Masoko
Anuani ya Posta: 160
Simu: 0672365354
Simu: 0672581557
Barua pepe: ded@kilwadc.go.tz /ictsupport@kilwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa