Mkuu wa Wilaya ya Kilwa Mkoa wa Lindi, Mhe. Christopher Ngubiagai amewaasa Wananchi Wilayani humo kujiunga na Mifuko ya afya ili wajiandae kutibiwa kirahisi pindi wakipata magonjwa.
Ngubiagai alitoa wito huo jana alipokuwa anazungumza na wananchi wa kijiji cha Nakiu kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji hicho kikichopo katika kata na tarafa ya Nanjirinji.
Mkuu huyo wa Wilaya alisema inashangaza kuona watu wengi wakitumia nguvu kubwa kufanya maandalizi ya sherehe.Ikiwamo harusi.Huku wengine wakiwa mahodari kuchangia rambirambi badala ya matibabu ya wagonjwa.
Alionya kuwa tabia hiyo haifai kufanywa na watu wanaojitambua.Badala yake wajenge utamaduni wa kujali afya zao kwa kuchukua tahadhari mapema.Ikiwamo kujiunga na mifuko ya afya ambayo itawafanya watibiwe wakati wote.Hivyo kuondoa usumbufu wa vikao vya kuchangishana fedha kwa ajili ya matibabu pindi wanaumwa.
Alisema hauzuii watu kufanya maandalizi ya sherehe wala kutoa fedha kwa ajili ya mazishi na rambirambi.Bali waanze kujali afya zao ili wawaondolee mzigo jamaa zao pindi wanapoumwa au wasitumie fedha nyingi kwa ajili ya matibabu wakati serikali imewarahishia upatikanaji huduma za matibabu kwa gharama nafuu.
Alisema katika kuthibitisha serikali imeamua kuboresha huduma za afya kwa ajili ya wananchi wake.Ikiwemo kuongeza dawa na vifaa tiba kwenye zahanati,vituo vya afya na hospitali.Huku bajeti ya wizara yenye dhamana ya afya inapanda kila mwaka.
"Wilaya ya Kilwa imepokea shilingi 1.5 bilioni kwa ajili ya ukarabati wa vituo vya afya.Pia inatarajia kupokea shilingi 500 milioni kwa kazi hiyo.Tayari tumeletewa watumishi 104 wa sekta ya afya.Hivi unawezaje kushindwa kujiunga na mifuko hiyo kwa gharama nafuu wakati huo unatumia fedha nyingi kuandaa harusi huku ukijua bibi harusi na bwana harusi wataumwa na kuhitaji tiba,"alisisitiza nakuhoji Ngubiagai.
Katika kuhakikisha wanaojiunga na mifuko hiyo(CHF na NHIF) wanafaidika.Ngubiagai amewaagiza watumishi wa idara ya afya kuwapa kipaumbele wagonjwa waliojiunga na mifuko hiyo.Badala ya wanaokwenda na fedha taslimu.Huku akitoa wito kwa wananchi kumpa taarifa za mwenendo wa upatikanaji huduma kwenye vituo vya afya,zahanati na hosipitali.
Kwa upande wake mratibu wa CHF wilaya ya Kilwa,Fred Mpondachuma aliwaondoa hofu wananchi kuhusu uhakika na ubora wa matibabu kwenye zahanati,vituo vya afya na hosipitali kwa watu waliojiunga na mifuko ya afya.Kwani zimeboreshwa na dawa zinapatikana kwa wingi.
Alisema uboreshwaji wa huduma za afya nchini umeondoa dhana yamuda mrefu ya kuamini hospitali za nje ya nchi.Kwasababu hata viongozi wa kitaifa na familia zao wameanza kutibiwa hapa nchini.Kwasababu hata baadhi ya magonjwa ambayo yalikuwa tiba zake zilikuwa zinapatikana nje ya nchi yameanza kutibiwa nchini.
Katika hatua nyingine Ngubiagai amewapa siku 14 viongozi wa serikali ya kijiji hicho wawewamempatia idadi ya wafugaji na mifugo iliyopo katika kijiji hicho ili amalize mgogoro baina ya wakulima na wafugaji katika kijijji hicho.Huku akiweka wazi kwamba baadhi ya watendaji na viongozi wa serikali wilayani humo wanachangia migogoro kwasababu ya kupindisha sheria kwasababu ya tamaa.
NEWS CREDIT : MUUNGWANA BLOG
Kilwa Masoko
Anuani ya Posta: 160
Simu: 0672365354
Simu: 0672581557
Barua pepe: ded@kilwadc.go.tz /ictsupport@kilwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa