Katika kuhakikisha utekelezaji wa kauli mbiu ya siku ya Wanawake Duniani inayosema “WANAWAKE NA WASICHANA 2025 TUIMARISHE, HAKI, USAWA NA UWEZESHAJI”. Mkuu wa Wilaya ya Kilwa Mhe. Mohamed Nyundo, Amewataka wanawake Wilayani Kilwa kufata fursa zinazoweza kuwainua kiuchumi ikiwemo kupata mikopo yenye riba nafuu kutoka Taasisi za Kibenki na Mikopo isiyo na riba inayotolewa na halmashauri ili iweze kuwainua katika shughuli zao za ujasiliamli na uchummi kwa ujumla.
Mhe. Nyundo ameyaeleza hayo tarehe 07/03/2025 katika Maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani ambapo Kiwilaya yamefanyika katika Kijiji cha Zinga Kibaoni Kata ya Miguruwe ambapo pia alipata nafasi ya kufanya Ufunguzi wa Nyumba ya kulala wageni iliyojengwa na mfanya biashara anayejihusisha na shughuli za ufugaji aitwae Maduka Shija Golani katika kijiji hicho.
Aidha Mhe. Nyundo Amewaomba wanawake na jamii kwa ujumla kuwekeza katika katika Elimu kupitia kusomesha watoto wa kike ili waweze kufikia malengo yao, pia amewataka kujitokeza katika kugombea nafasi mbalimbali za uongozi kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.
Akiwasilisha Risala kwa niaba ya Umoja wa Wanawake Wilaya Kilwa Bi. Mwanaidi Salo amesema moja ya changamoto ya kufikia malengo ya maendeleo endelevu ya mwaka 2030 kwa wanawake ni ukatili ya kijinsia unaojitokeza katika jamii. Hivyo wameandaa Jukwaa la wanawake liitwalo Tumaini Jipya la Wanawake Kilwa (TUJIWAKI) ambalo linasaidia katika utetetezi wa Wanawake na watoto na kutoa elimu kuhusiana na ukatili wa kijinsia.
Pia Bi. Mwanaidi amemshukuru Mkuu wa Wilaya ya Kilwa, kwa kusimamia ulinzi na usalama wa Wilaya ya hiyo ambao unapelekea Halmashauri na wadauu mbalimbali wa Maendeleo ikiwemo Kampeni za msaada wa Kisheria wa Mama samia na Dawati la kijinsia kwa kufanya jitihada za kuondosha na kupambana na changamoto za ukatili wa kijinsia.
Kilwa Masoko
Anuani ya Posta: 160
Simu: 0672365354
Simu: 0672581557
Barua pepe: ded@kilwadc.go.tz /ictsupport@kilwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa