Mkuu wa Wilaya ya Kilwa Mhe. Nyundo ameelekeza kitengo cha uvuvi ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa kuwahamasisha wananchi wanaojihusisha na shughuli za uvuvi wilayani Kilwa, kujiandaa na fursa zitakazotokana na mradi wa Bandari ya uvuvi ikiwemo kujipatia ajira katika Bandari hiyo.
Akitoa maelekezo hayo 30 Januari 2025 katika Mkutano wa Baraza la Ushauri Wilayani Kilwa (DCC) ambao umejadili Rasimu na Mpango wa Bajeti kwa Mwaka wa Fedha 2025/2026 amesema kuwa wananchi Wilayani Kilwa wanatakiwa kufanyia kazi fursa zinazokuja mbele yao na si kusubili maelekezo kutoka kwa Serikali.
Kwa upande wao Wajumbe wa Baraza hilo wameishauri jamii Wilayani Kilwa, hususani wanaojihusiha na shughuli za Uvuvi, kuangalia fursa ya Bandari ya uvuvi kwa jicho la tatu, ikiwemo kutafuta elimu katika vyuo vinavyofundisha elimu ya Bahari na Uvuvi, ili kuwawezesha kupata vyeti vitakavyosaidia kupata nafasi, pindi ajira zitakapotangazwa katika Bandari hiyo.
Kilwa Masoko
Anuani ya Posta: 160
Simu: 0672365354
Simu: 0672581557
Barua pepe: ded@kilwadc.go.tz /ictsupport@kilwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa