Mkuu wa Wilaya ya Kilwa, Mhe. Mohamed Nyundo, tarehe 13, Juni2025 ametembelea mabanda mbalimbali ya maonesho ya madini na fursa za uwekezaji katika LINDI MINING EXPO 2025 yanayoendelea kufanyika Wilayani Ruangwa, Mkoa wa Lindi.
Akiwa katika ziara hiyo, Mhe. Nyundo amepata fursa ya kujionea ubunifu, teknolojia na miradi mbalimbali ya madini inayotekelezwa na taasisi, kampuni binafsi pamoja na Halmashauri kutoka mikoa ya kusini mwa Tanzania. Maonesho hayo yanalenga kuhamasisha ushiriki wa wananchi na wawekezaji katika sekta ya madini kama njia ya kukuza uchumi wa mkoa na taifa kwa ujumla.
Pia Mhe. Nyundo ameipata maelezo kutoka kwa wataalamu wa sekta ya madini kuhusu miradi inayoendelea na mikakati ya kuvutia wawekezaji. Aidha, alizungumza na wadau wa sekta hiyo ambapo alihimiza ushiriki wa wananchi katika kunufaika na rasilimali zilizopo kupitia ushirikiano baina ya sekta binafsi na serikali za mitaa.
Kaulimbiu ya mwaka huu ni
“Madini na Uwekezaji Fursa ya Kiuchumi Lindi – Shiriki Uchaguzi Mkuu 2025”, ikisisitiza umuhimu wa ushiriki wa wananchi katika maendeleo ya kiuchumi kupitia sekta ya madini sambamba na uwajibikaji wa kiraia katika uchaguzi mkuu ujao.
Aidha Mhe. Nyundo alisisitiza kuwa Wilaya ya Kilwa imejipanga kikamilifu kunufaika na fursa zinazotokana na sekta ya madini kwa kuweka mazingira rafiki kwa wawekezaji na kuhakikisha wananchi wanashiriki kikamilifu katika shughuli za kiuchumi.
Kilwa Masoko
Anuani ya Posta: 160
Simu: 0672365354
Simu: 0672581557
Barua pepe: ded@kilwadc.go.tz /ictsupport@kilwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa