Mkuu wa Wilaya ya Kilwa Mhe. Mohamed Nyundo amefanya kikao kazi na Maafisa Kilimo pamoja na Mameneja wa vyama vya Msingi (AMCOS) Wilayani humo kwa lengo la kutoa maelekezo juu ya udhibiti na utunzaji wa ubora wa korosho zinanopelekwa magharani hususani ghara la Nangurukuru. Kikao hicho kimefanyika katika ukumbi wa Chuo cha Maendeleo ya Jamii Kilwa Masoko leo 17/10/2024.
Aida Mhe. Nyundo ameeleza kuwa uhifadhi mbaya wa korosho ni sababu kuu inayopelekea kushuka kwa thamani ya korosho kwani jambo hilo linapelea korosho kupata unyevunyevu, kuoza au kupoteza ladha yake. Hivyo amewataka Maafisa Kilimo na Meneja wa Vyama Vya Msingi AMCOS, kuhakikisha maghara yanafungwa kwa kufuli mbili jioni na kila mmoja wao anakuwa na funguo na kufungua kwa pamoja asubuhi, ili kudhibiti uingizaji kinyemela wa korosho zisizo na ubora nyakati za usiku.
Kilwa Masoko
Anuani ya Posta: 160
Simu: 0672365354
Simu: 0672581557
Barua pepe: ded@kilwadc.go.tz /ictsupport@kilwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa