Mkuu wa Wilaya ya Kilwa Mhe. Mohamed Nyundo amewataka Wananchi kushirikiana na Viongozi hususani wa Viongozi wa Dini katika kudumisha Amani na Usalama uliopo Kilwa. Ametoa nasaha hiyo baada ya kupata Futari na Wakuu wa Idara, Viongozi Mbalimbali na Wananchi Nyumbani kwake, jana jioni Tarehe 21/03/2025.
Pia ametoa Shukrani kwa kwa Viongozi hao na Wananchi kwa ushirikiana nae katika masuala mbalimbali ya Kijamii ikiwemo tukio hilo la Kupata Futari kwa pamoja katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhan.
Kilwa Masoko
Anuani ya Posta: 160
Simu: 0672365354
Simu: 0672581557
Barua pepe: ded@kilwadc.go.tz /ictsupport@kilwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa