Kilwa,
Kamati ya ulinzi na usalama Wilayani Kilwa kwa Kushirikiana na Bodi ya Michezo ya Kubahatisha imekamata na kuteketeza Mashine 63 ambazo zilikua zimewekwa sehemu zisizo rasmi na kuendeshwa kinyume na sheria.
Akizungumza kabla ya kuteketeza Mashine hizo Afisa Mkaguzi wa Michezo ya Kubahatisha kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Ndg. Jehud Ngolo amesema Uongozi wa Wilaya ya Kilwa uliwasilisha barua kwa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha juu ya Kukithiri kwa michezo ya kubahatisha Wilayani Kilwa isiyozingatia taratibu na Sheria.
“Sheria zilizokiukwa ni pamoja na Kutokuwa na Leseni za maeneo Husika kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha (Site Licences) na baadhi ya Mashine Kukosa Stika yaani Mashine Bandia” alisema Ngolo
Ngolo amesema Kifungu 82 cha Gaming Act, 2003 kama ilivyorekebishwa na Kifungu 82A cha Finance Act, 2015 kinaipa Mamlaka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha (Gaming Board of Tanzania) kukamata na kuteketeza Mashine husika.
Amesema Kifungu 77 cha Sheria ya Michezo ya kubahatisha inawataka Waendeshaji wa michezo ya kubahatisha kuhakikisha Vifaaa (Mashine za Bahati nasibu) vimeidhinishwa na kusajiliwa kwani kinyume na hapo yanaweza kutokea Madhara ikiwemo Watoto kushiriki kwa kua hakuna uangalizi unaotambulika kisheria, Mashine zinazotumika zinaweza kuwa chini ya kiwango pamoja na kukosekana kwa usalama wa Wachezaji.
Jumla ya Mashime 63 zikiteketea kwa Moto baada ya kukamatwa na Bodi ya Michezo ya kubahatisha kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi Wilayani Kilwa (Picha: Ally Ruambo)
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kilwa ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na usalama amempongeza Mkurugenzi wa Bodi ya Michezo ya kubahatisha kwa hatua alizochukua baada ya kupokea barua ya malalamiko juu ya utitiri wa Mashine za kubahatisha zilikuwa zikiendeshwa kinyume na sheria.
Pia Ngubiagai amewataka vijana Wilayani Kilwa na Taifa kwa ujumla kujishughulisha na shughuli za kimaendeleo na kuacha mawazo ya kutegemea michezo ya bahati nasibu pekee katika kubadilisha maisha yao.
“Ingawa hii Michezo inajulikana Kisheria lakini ni vyema wakatumia muda wao mwingi katika shuguli za kimaendeleo, wafanye kazi halali kama ni kilimo, biashara, ujasiriamali nakadhalika ili kusudi waweze kupata mapato ambayo yatawasaidia katika kujenga masha yao na uchumi wa Taifa kwa ujumla”
Aidha Ngubiagai ameahidi kuendelea kutoa ushirikiano kwa Bodi ya Michezo ya kubahatisha na kumpongeza Mkuu wa Polisi Wilaya ya Kilwa na timu yake kwa ushirikiano walioutoa kwa Bodi ya Michezo ya kubahatisha kuanzia mwanzo mpaka mwisho wa zoezi na kuagiza zoezi hilo liwe endelevu.
Mkuu wa Wilaya ya Kilwa (Katikati) akizungumza na Waandishi wa Habari kabla ya zoezi la kuteketeza Mashine zilizokamtwa na Bodi ya Michezo ya kubahatisha kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi Wilayani Kilwa, wa kwanza kushoto Ndg. Bakari Maggid , kulia Ndg. Jehud Ngolo Maafisa ukaguzi wa michezo ya kubahatisha (Picha : Ally Ruambo)
Jumla ya mashine 63 zikiwemo 45 za kampuni ya Bonanza, 15 JX Betting na 3 Mashine Bandia zimekamatwa wilayani Kilwa zikiwa zimewekwa maeneo yasiyo ruhusiwa kisheria, kwa mujibu wa Sheria Mashine hizo zinaruhusiwa sehemu za kuuzia vileo kama vile Baa,Pabu na kwenye grosari.
Kilwa Masoko
Anuani ya Posta: 160
Simu: 0672365354
Simu: 0672581557
Barua pepe: ded@kilwadc.go.tz /ictsupport@kilwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa