Wizara ya Mifugo na Uvuvi kupitia Taasisi ya Uhifadhi wa Bahari na Maeneo Tengefu Tanzania (MPR) imetoa Mafunzo kwa Viongozi wa BMU Kilwa (Beach Management Unit) kuhusiana na faida za Uchumi wa buluu ili kuwajengea uelewa juu ya mpango wa kuanzisha uhifadhi na maeneo tengefu katika wilaya Kilwa ikiwa ni moja ya jitihada za kukuza sekta ya Uvuvi katika Wilayani Kilwa.
Akiwa katika ufunguzi wa Mafunzo Hayo Katibu Tarafa Wilayani Kilwa Mhe. Yusuf Mkomi amesema kuwa Uhifadhi unaoendana kuanzishwa katika Wilaya Kilwa utaenda kusaidia kukuza utalii hususani katika suala la zima la utunzaji wa fukwe za bahari kwaajiri ya shughuli za kitalii.
Kikao hicho kilichofanyika tarehe 16 Januari 2025 katika ukumbi wa Chuo Mandeleo (FDC) Kilwa kimewakutanisha Viongozi kutoka Taasisi 29 za BMU Wilayani Kilwa ambapo Mwezeshaji wa mafunzo hayo Ndg. Godfrey Ngupola amesema Uhifadhi na maeneo tengefu Kilwa utasaidia kuwepo kwa mpangilio wa maeneo ya madharia ya Samaki kupangwa kimatumizii na kuleta faida endelevu kwa wananchi ukitofautisha na Uvuvi wa kawaida ambao unatumika katika Jamii.
Aidha Ndg. Ngupula ameongeza kuwa mpango huo utasaidia wananchi kujipangia utataratibu wa kutumia rasilimali ndani ya eneo la hifadhi kufanyiwa tafiti za mara kwa mara na kulindwa rasmi kwa utaratibu maalumu njia hiyo itasaidia kupunguza Uvuvi usio na utaratibu maalumu na wizi wa samaki kipindi cha ufungaji wa mwamba darasa.
Kwa upnde wake Afisa uvuvi Mkoa Ndg.Jumbe Kawambwa amesema mpango huo wa uhifadhi wa maeneo tengefu pia umelenga kuleta maendeleo kupitia Bandari ya Uvuvi hususani katika kuongezeka uvunaji wa samaki kupitia Elimu ya uhifadhi na utunzaji wa madharia ya samaki itakayo tolewa kwa wananchi kupitia mafunzo hayo.
Sambamba na hilo Ndg.Kawambwa ametoa wito kwa kwa wananchi kushirikiana na Wizara ya Ufugaji na Uvuvi katika utekezaji ili kuhakikisha mpango huo unakamilika kama ulivyokusudia
Kilwa Masoko
Anuani ya Posta: 160
Simu: 0672365354
Simu: 0672581557
Barua pepe: ded@kilwadc.go.tz /ictsupport@kilwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa