• Malalamiko |
    • Anuani Zetu |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
Kilwa District Council
Kilwa District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Mikakati ya Halmashauri
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Afya
      • Utumishi na Utawala
      • Elimu ya Msingi
      • Mipango na Takwimu
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Ujenzi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Mifugo na Uvuvi
      • Fedha na Biashara
      • Maliasili
    • Vitengo
      • Usafi na Mazingira
      • Sheria
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Uchaguzi
      • Ugavi
      • TEHAMA
      • Nyuki
      • Biashara
      • TASAF
      • Lishe
      • Uvuvi
    • Miji Midogo
      • Masoko
      • Kivinje
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Huduma za Uwekezaji
    • Biashara na Viwanda
    • Madini
    • Uvuvi
    • Utalii
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
    • Mikopo kina Mama na Vijana
    • Huduma za Maji
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Uchumi Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
    • Ratiba ya Vikao vya Kisheria
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Itakayo tekelezwa
  • Machapisho
    • Muongozo
    • Utaratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Picha
    • Habari
    • Matukio
  • Mifumo
    • PlanRep
    • FFARS
    • Prem
    • Salary Slip Portal

BIL. 296 ZATENGWA KUKAMILISHA ZOEZI LA UCHANJAJI WA MIFUGO NCHINI

Posted on: August 8th, 2025

Mifugo laki 3 yatarajiwa kufikiwa na kuchanjwa Mikoa ya Lindi na Mtwara.

Serikali imetenga zaidi ya shilingi bilioni 296 kwa ajili ya utekelezaji wa zoezi la uchanjaji wa mifugo nchini, ikiwa ni sehemu ya jitihada za kudhibiti magonjwa hatari yanayopunguza tija kwa mfugaji na kuathiri upatikanaji wa soko la kimataifa.


Akizungumza katika Maadhimisho ya Siku ya Mifugo na Uvuvi, Tarehe 8 Agosti 2025 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Dkt. Edwin Mhede, amesema serikali imepanga kufikia lengo la kuchanja asilimia 70 ya mifugo yote nchini ifikapo Oktoba 2025.


Kwa mujibu wa takwimu, jumla ya ng’ombe wanaokadiriwa kuwapo katika mikoa ya Lindi na Mtwara ni zaidi ya mifugo laki tatu na ambao nao wanatarajiwa kufikiwa na zoezi hilo, huku ikitarajiwa kuwa miongoni mwa mikoa inayotarajiwa kutekeleza kwa ufanisi zoezi hilo.


“Magonjwa yasipodhibitiwa huathiri kwa kiasi kikubwa thamani ya mifugo katika soko hasa la kimataifa. Serikali imeweka msukumo ili kuhakikisha zoezi hili linafanyika kwa ufanisi ili kufikia viwango vinavyokubalika kimataifa ili kuleta tija kwa mfugaji pamoja na kudhibiti tatizo la uwizi wa mifugo” alisema Dkt. Mhede.


Vilevile, Dkt. Mhede amesema kuwa serikali ya awamu ya sita inaendelea na mpango wake wa kuwawezesha wananchi kupitia sekta za kimkakati ikiwemo Kilimo, mifugo na uvuvi kwa kuongeza msukumo ili kuhakikisha kuwa wananchi wote wanafikiwa na sekta hizi za kimageuzi, Katika upande wa uvuvi, serikali inaendelea kuwawezesha wavuvi wa ukanda wa pwani kwa kuwapatia boti za kisasa kupitia mikopo isiyo na riba, ili kuongeza tija katika shughuli zao na kuchochea uchumi wa buluu, na wakulima wakiendelea kunufaika na utolewaji wa pembejeo za kilimo bure.


Aidha, kupitia maadhimisho hayo, Dkt. Mhede amewakumbusha wananchi kuzingatia ulaji wa lishe bora, hasa protini zinazotokana na wanyama, huku akisisitiza matumizi ya bidhaa za mwani kwa afya na tiba, zikiwemo mafuta, unga na mbolea ya mwani pamoja na kuzitaka halmashauri kushirikiana na wataalamu kutoka idara za afya, lishe na maendeleo ya jamii ili kuhakikisha wananchi wananufaika na jitihada hizi za serikali katika kuboresha maisha yao.

Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI HALMASHAURI YA WILAYA YA KILWA September 03, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI September 27, 2024
  • TANGAZO KWA UMMA KUHUSU UTOAJI WA MIKOPO KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU October 04, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI October 11, 2024
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • KILWA DC YAANZA KWA KISHINDO SHIMISEMITA

    August 16, 2025
  • MTANDAO WA BMU WAELEZA FAIDA ZA ZIARA YA MAFUNZO MKOANI TANGA

    August 15, 2025
  • DED NA TIMU YA UFUATILIAJI KILWA WAFANYA UKAGUZI WA MIRADI YA MAENDELEO

    August 14, 2025
  • KAMATI ZA MAANDALIZI YA SHEREHE ZA MAJIMAJI KILWA ZAKUTANA KUJADILI MAANDALIZI YA SHEREHE HIZO

    August 13, 2025
  • Tazama Zote

Video

Mkuu wa Wilaya ya Kilwa Akipokea Mwenge wa Uhuru.
Video Zaidi

Kurasa za Haraka

  • TARURA GPN
  • Watumishi Portal
  • MIKOPO 10%
  • Mikopo ya Wanawake na Vijana
  • Huduma za Elimu

Tovuti Muhimu

  • Utumishi
  • Tamisemi
  • Ikulu
  • Wizara ya Fedha
  • Wizara ya Elimu
  • Lindi

Idadi ya Watembeleaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Watembeleaji

writingMasterThesis

Ramani ya Mahali

Anuani Zetu

    Kilwa Masoko

    Anuani ya Posta: 160

    Simu: 0672365354

    Simu: 0672581557

    Barua pepe: ded@kilwadc.go.tz /ictsupport@kilwadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Kanuni Binafsi
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa