Wajumbe wa Baraza Ushauri Wilayani Kilwa wameshauri kuongezwa kwa udhibiti wa migogoro ya ardhi kati ya Wakulima na Wafugaji ili iwe sehemu ya kudumisha zaidi Amani na Usalama Wilayani Kilwa. Hayo yamezungumzwa wakati wa Mkutano wa Baraza la Ushauri Wilaya ya Kilwa (DCC) uliofanyika katika ukumbi wa Sultani Masoko Tarehe 30/01/2025 ili kujadili Rasimu na Mpango wa Bajeti kwa Mwaka wa Fedha 2025/2026.
Akizungumza katika Mkutano huo Mkuu wa Wilaya ya Kilwa Mhe. Mohamed Nyundo amesema hatua zilizoundwa za kutatua migogoro kati ya wakulima na wafugaji Wilayani Kilwa ni udhibiti wa uingiaji wa mifugo katika maeneo mbalimbali wilayani humo, pia kuandaa maeneo maalumu kwaajiri ya wakulima na wafugaji ili kuondoa muingiliano utakaopelekea kutokea kwa migogoro hiyo.
Aidha Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Kilwa Ndg. Shija Lyella amesema kuwa katika udhibiti wa migororo ya wakulima na wafugaji tayari Halmashauri imeandaa wataalamu watakaosaidia kuendesha ranchi za wafugaji ili kupunguza migogoro hiyo.
Sambamba na hayo Mhe. Nyundo amewaelekeza wataalamu wanaohusika na Bajeti kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa, kuongeza mshikamano na taasisi mbalimbali katika uandaaji wa bajeti na utekelezaji wa miradi ili kupunguza matumizi ya fedha na kurahisisha utekelezaji wa miundombinu katika muda uliopangwa.
Kilwa Masoko
Anuani ya Posta: 160
Simu: 0672365354
Simu: 0672581557
Barua pepe: ded@kilwadc.go.tz /ictsupport@kilwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa