Mwenyekiti wa Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa, Mhe.Farida Kikoleka, amesema tayari Halmashauri imeagiza Wataalamu kutoka Idara ya Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira kwenda katika maeneo yenye changamoto kubwa ya uharibifu unaotokana na wanyamapori,kwa lengo la kuwasaidia wananchi kupambana na changamoto hizo. Hayo yamezungumzwa wakati wa Mkutano wa Baraza la Madiwani uliofanyika katika katika ukumbi wa Chuo Cha Maendeleo ya Wananchi (FDC) Kilwa Tarehe 03/02/2025.
Aidha, Wahe. Madiwani wamewapongeza timu ya wataalamu wa Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa kwa kushirikiana na Taasisi zinazaohusika na Mwanyapori ikiwemo TAWA na TANAPA kwa juhudi zinazofanyika ili kuondoa au kumaliza uharibifu unaotokana na wanyamapori, Pia wametoa wito kwa Halmashauri Kuongeza Vitendea Kazi kwa Wataalamu hao ikiwemo Vyombo vya Usafiri Ili Waweze Kufanya Kazi zao kwa Ufanisi.
Kwa upande wake Katibu Tawala wa Wilaya ya Kilwa Mhe. Yusuf Mwinyi amesema tayari mazungumzo yamefanyika baina ya Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kilwa na Ofisi ya TANAPA yanayohusu kuinua Sekta ya Utalii Wilayani Kilwa sambamba na Ujenzi wa Kituo kikubwa cha kuthibiti Wanyapori katika eneo la Likawage Wilayani Kilwa. Hatua hiyo ni moja ya mbinu za kuondoa athari na uharibifu unaosababishwa na wanyamapori.
Kilwa Masoko
Anuani ya Posta: 160
Simu: 0672365354
Simu: 0672581557
Barua pepe: ded@kilwadc.go.tz /ictsupport@kilwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa