Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Dkt. Edwin P. Mhede leo tarehe 07 Agosti 2025, ametembelea Banda la Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa katika Maonesho ya Nanenane Kanda ya Kusini, ambapo ameridhishwa na maandalizi yaliyofanyika na namna banda hilo lilivyoandaliwa kwa ubora.
Dkt. Mhede amepongeza juhudi za halmashauri kwa kuandaa banda lenye mazao bora ya kilimo, bwawa la samaki lililoandaliwa kitaalamu pamoja na mifugo yenye ubora.
Aidha, amefurahishwa na ushiriki wa wajasiriamali wanaoonyesha bidhaa mbalimbali zitokanazo na kilimo, mifugo na uvuvi, akisisitiza kuwa huo ni mfano mzuri wa mnyororo wa thamani unaopaswa kuendelezwa.
Kilwa Masoko
Anuani ya Posta: 160
Simu: 0672365354
Simu: 0672581557
Barua pepe: ded@kilwadc.go.tz /ictsupport@kilwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa