Katibu Tawala wa mkoa wa Lindi Bi. Zuwena Omary ameipongeza Halmashauri ya wilaya ya Kilwa kwa kupata Hati safi (Unqualified Opinion) kwa kipindi cha miaka mitano mfululizo kuanzia mwaka 2018\2019 hadi 2022\2023
Ameyasema hayo katika baraza la kujadili hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kilichofanyika katika ukumbi wa PEC uliopo Kilwa Masoko, ambapo amesema kuwa ukaguzi huo unafanywa kwa lengo la kubaini matumizi sahihi ya fedha za serikali.
Hata hivyo, kutokana na Halmashauri hiyo kuwa na Hati safi kwa vipindi vyote hivyo ametoa rai kwa Watendaji wote wa wilaya hiyo kuwa na ushirikiano ili kuilinda heshima waliyopata kwa kuendelea kuapata hati safi Zaidi ikiwemo kuchukua hatia kwa hoja zinazoibuliwa na Wakaguzi wa ndani na kuzifanyia kazi kwa wakati ambapo itasaidia kupunguza hoja za kujibu au kutokuwepo kabisa
Aidha, Bi Zuwena amewataka viongozi pamoja na Watendaji wote kuwajibika katika majukumu ikiwemo utakelezaji wa miradi ya maendeleo kwa wakati, hii itafanya fedha za serikali kutumika katika matumizi sahihi ambapo itasababisha hoja za Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali kuwa chache.
Mwisho, Ametoa rai kwa viongozi kuendelea kujiandaa na uchaguzi wa Serikali za Mitaa pamoja na Uchaguzi Mkuu ikiwemo kutoa elimu ya Wapiga kura kuhusu kujiandikisha katika Daftari la kudumu la Mpiga kura, kushiriki katika Kampeni pamoja na kupiga kura kwani ni haki yao Kisheria.
Kilwa Masoko
Anuani ya Posta: 160
Simu: 0672365354
Simu: 0672581557
Barua pepe: ded@kilwadc.go.tz /ictsupport@kilwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa